Followers

Njia sita 6 za kumfanya Mtu aweze kujiamia kwa asilimia 100



Kila kitu ambacho ni halisi kinawezekana. Bila shaka unakumbuka vizuri kuhusu namna kutojiamini kwetu kunavyojengwa. Kwa kuwa tunajua chanzo, ni rahisi kupata tiba.

Njia zifuatazo zinaweza kukusaidia katika kujenga kujiamini.Kuna njia nyingi zinazopendekezwa, lakini kuna zile ambazo zimetumika sana katika kufanya kazi hiyo.

 Hizi zifuatazo ni baadhi yake.

1. Yachunguze mawazo yako na vitendo vyako kwa uangalifu ili kujua ni kitu gani hukufanya usisimke.
Anza kufanya mambo ambayo unaona kwamba una uwezo kuyafanya bila wasiwasi na kuchukua uamuzi unaojitegemea kufuatana na utashi wako. Ikibidi unaweza kuomba msaada wa wengine, lakini jaribu kila mara kufanya mambo kufuatana na unavyoyaona.

2. Jifunze kujithamini.
Inawezekana kwa miaka na miaka umekuwa unajiona kama mtu usiye na thamani. Pia unaweza ukaona kwamba, hadhi uliyokuwa nayo mbele ya ndugu, jumuiya na jamii imepungua. Jali ujuzi na vipaji vyako; hata kama kuna ndugu wametajirika pamoja na kuwa ni mbumbumbu hiyo isiwe chanzo cha kukuvunja nguvu. Iko siku utafanikiwa kama utaanza kujiamini.

3. Jisamehe bila masharti yoyote.
Kama maisha yako ya awali yalikuwa si ya kiungwana, jisamehe na anza maisha yako upya. Njia bora ya kujisamehe ni kujipenda bila masharti yoyote.

4. Pambana na hofu.
Hofu ni kitu kibaya sana kwa sababu inaingilia kwenye uwezo wako wa kufikiri. Ili ufanikishe malengo yako ya maisha huna budi kuhakikisha kuwa huna hofu tena.

5. Fanya vitu unavyoviogopa.
Orodhesha idadi ya vitu ambavyo ulikuwa unaviogopa. Kisha anza na vitu ambavyo unaviogopa zaidi na jiulize kwa nini usiweze kuvifanya.

6. Jifunze kupambana na kushindwa.
Kubali kwamba kushindwa ni kama chombo cha kujifunzia na si kitu cha kukukatisha tamaa. Jua, na amini kwamba, bila kushindwa hakuna kukua. Pia elewa kwamba, kushindwa siyo dalili ya udhaifu, bali uimara.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.