Followers

RC TABORA ATOA DILI KWA BODABODA KWA WANAOTUPA TAKA HOVYO BARABARANI KILA KICHWA ELFU 25


Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Agrey Mwanri ameamua kutoa ajira kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda mkoa wa Tabora katika kampeni yake ya utunzaji wa mazingira mkoani hapa, Rc Mwari  ametangaza wazi kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora mara bada ya Sheria kuwekwa Mkoani hapa kwa yeyote atakae bainika amechafua mazingira kwa kutupa taka barabarani au sehemu isiyostahili kama Vituo vya Mabasi na Daladala,Barabarani,Sokoni n.k atakamatwa na kufikishwa Mahakamani ikiwa ni pamoja na kutozwa faini kiasi cha shilingi Eflu Hamsini(50,000/=)

Katika juhudi za kutunza mazingira na kuhamasisha wananchi wa Manispaa ya Tabora kutunza mazingira Rc Mwanri ameamua kutoa fursa kwa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda kushirikiana na Serikali kuhakikisha mji unakuwa safi na salama na kila mmoja anakuwa mlinzi wa mwenzake, Ili kufanikisha zoezi hilo Rc Mwanri ametoa motisha kwa Madereva hao wa Pikipiki kuwa atakaye mkamata mtu akitupa taka sehemu yoyote hasa katika barabara na sehemu za vituo vya magari na pikipiki na kumfikisha eneo husika atapokea shilingi elfu ishirini na tano (Tsh.25.,000/=) kati ya Elfu 50 atakayo tozwa mchafuzi wa mazingira

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.