Siri 39 za kuwa Milionea, Jinsi ya kupata pesa na kuwa tajiri
DOWLOAD APP YA SUPERNIDA BLOG KWENYE SIMU YAKO ILI KUPATA HABARI ZETU ZOTE KWA HARAKA NA RAHISI ZAIDI, BONYEZA HAPA
Siku ya leo naomba nikupe siri kubwa ambazo zitakufanya wewe uweze kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha yako, na siri hizi zitakufanya uwe ni mtu mwenye endapo utaamua kuzifanyia kazi. Na siri hizi ni
1. Tafuta fursa kila kona.
2. Tumia kipaji chako.
3. Kuwa na nidhamu katika fedha - matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.
4. Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyote - kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.
5. Usipoteze muda - jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
6. Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.
7. Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.
8. Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali duniani - soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.
9. Jenga urafiki na taasisi za kifedha - mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha - tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.
10. Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.
11. Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo.
12. Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali.
13. Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa - angalia fursa hapo ulipo na wekeza.
14. Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako.
15. Chunguza jamii yako wanakosa bidhaa gani kisha dili na bidhaa hiyo nawe utakuwa milionea.
16. Kuwa na wazo (Business idea): mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.
17. Fanya vitu wewe mwenyewe - acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu.
18. Kuwa na malengo - kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.
19. Kuwa na moyo wa ujasiri - usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.
20. Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.
21. Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.
22. Fanya vitu kitofauti; fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.
23. Acha woga - jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.
24. Kuwa na mtazamo chanya - usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
25. Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.
26. Kuwa na mipaka katika mambo yako - usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu.
27. Dili na watu wenye kipato kidogo na kati katika biashara zako; mamilionea wengi hulenga mahitaji ya watu wa hali ya chini ambao ndio wengi hapa duniani. Baadhi ya mahitaji ya watu wa hali ya chini ni;
(a) Vyakula na vinywaji.
(b) Vifaa vya ujenzi.
(c) Vifaa vya umeme.
28.Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.
29. Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako - waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
30. Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.
31. Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe.
32. Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja.
33. Ubunifu ni muhimu sana - fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini - kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.
35. Nunua hisa katika mabenki, makampuni mbalimbali: Mamilionea wengi hununua hisa hivyo humiliki mabenki na makampuni mbalimbali.
36. Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli.
37. Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea.
38. Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea - kila binadamu anaweza kuwa milionea.
39. Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa - kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemu nk.
DOWLOAD APP YA SUPERNIDA BLOG KWENYE SIMU YAKO ILI KUPATA HABARI ZETU ZOTE KWA HARAKA NA RAHISI ZAIDI, BONYEZA HAPA
No comments
Post a Comment