Followers

Usiruhusu Maisha Yako Yatawaliwe Na Mambo Haya Kabisa


 DOWLOAD APP YA SUPERNIDA BLOG KWENYE SIMU YAKO ILI KUPATA HABARI ZETU ZOTE KWA HARAKA NA RAHISI ZAIDI,                    BONYEZA HAPA

                                     Bofya Hapa


Ikiwa upo kwa ajili ya kutaka maisha ya mafanikio makubwa, yapo mambo ambayo hutakiwi kuyaruhusu kabisa yatawale maisha yako. Unapokuwa unaruhusu mambo haya yatawale maisha yako, hiyo inakuwa ni sawa na kuamua kuharibu maisha uliyonayo.

Ni wajibu na jukumu lako kuyajua mambo haya ambayo tunakwenda kuyajadili na kuyafanyia kazi. Je, mambo haya ni mambo gani ambayo hutakiwi kuyaruhusu yatawale maisha yako?

Twende pamoja tujifunze;-

Mambo yaliyopita.
Kwenye maisha yako usifanye kosa ukaruhusu maisha yako ya sasa au yajayo yakatawaliwa na mambo ambayo yamepita. Mambo ambayo yamepita ni tayari yamepita pasipo kujali yamekuumiza au hayajakuumiza.

Achana na kila kitu cha nyuma ambacho tayari kimeshapita, kwani hata ukiendelea kukibeba sana hakitakusaidia kitu zaidi utaendelea kuumia na kuharibu kesho yako. iwe kuna makosa ulifanya, ulifanyiwa kitu kibaya na wengine, achana na hiyo habari.

Kuendelea kukumbuka mambo ambayo tayari yameshapita hiyo ni sawa na kuendelea kuyapa nguvu mambo hayo. Kikubwa maisha yako anza kuyatengeneza hapo ulipo na mambo yaliyopita usiruhusu yatawale maisha yako tena.

Maoni ya watu wengine juu yako.
Jambo la pili, usiruhusu maisha yako yatawaliwe na maoni ya watu wengine. Watu wanaweza wakawa na maoni juu ya maisha yako ambayo hayaendani kabisa na malengo yako, kwa hiyo ikiwa utaamua kuyafata basi utakuwa unajipoteza wewe.

Ndio maana kabla hujafanya kitu unatakiwa kujiuliza unakifanya kitu kwa sababu yako au kwa sababu ya maoni ya wengine? Wapo watu ambao hawawezi kufanya kitu mpaka wasikilize maoni ya wengine wanasema nini.

Umezaliwa kwa sababu ya makusudi maalumu ambayo unatakiwa uyatimize. Sasa  makusudi hayo huwezi kuyatimiza kama maisha yako unayeendesha kwa kutumia maoni ya watu. Usijaribu kuishi kwa ajili ya maoni ya wengine sana, utakwama.

Mawazo yako hasi.
Yapo mawazo ambayo unayo na mawazo hayo yamekuwa yakikuzuai kwa muda mrefu sana kuweza kufanikiwa. Pengine umekuwa na mawazo ya kusema kwamba siwezi kufanikiwa kwa sababu hii au ile.

Ukiangalia mawazo hayo hayana ukweli ila yamekuwa yakikuzuia kufanikwa kwa sababu unavyojiwazia. Kama unajiwazia kwa ndani huwezi kufanikiwa  kwa sababu umezaliwa kwenye ukoo haujiwezi au kwa sababu huna bahati ni dhahiri hutaweza kufanikiwa.

Kwa jinsi ilivyo, kama hakuna kinachokuzuia ndani yako kuweza kufanikiwa, basi na hata nje hakuna kitu ambacho kitaweza kukuzuia kufanikkiwa hata iweje. Uamuzi unabaki kwako, kutokuruhusu mawazo ya kutokufanikiwa yakutawale, basi.

Mahusiano.
Kati ya kitu kimojawapo chenye nguvu sana katika maisha ni mahusianao. Ni hatari sana kujihusisha na mahusiano na mtu yeyote eti kwa sababu huna mtu. Hiyo nikiwa na maana unaingia kwenye mahusiano kwa sababu furaha pekee unaipata huko.

Kama wewe unaona mahusiano ndimo sehemu pekee ya kupata furaha na huwezi kupata furaha mpaka uwe kwenye mahusiano basi utakuwa kwenye wakati mgumu sana maana utakuwa unatawaliwa na mahusiano.

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba, unatakiwa uwe imara na kutengeneza furaha yako wewe mwenyewe bila kujali upo kwenye mahusiano au la. Ni rahisi kuingia kwenye mahusiano mabovu na kuharibu maisha ikiwa utakuwa na mahusiano ya hovyo.

Pesa.
Tunaposema usiruhusu pesa itawale maisha yako tukiwa na maana hii, si kwamba pesa ni mbaya au kwamba hutakiwi kuitafuta, hapana. Hapa kinacholengwa usije ukakubali ukafanya maamuzi kwa sababu una pesa.
Unachotakiwa kuelewa ni kwamba usiruhusu pesa, ikawa ndio inatawala maamuzi yako. Fanya mambo yako si kwa sababu ya pesa. Ifanye pesa ibaki kwako kama kitu cha kukusaidia na si kwa sababu una pesa kichwa kinaanza kuyumba hovyo hovyo.

Haya ndio mambo ya msingi ambayo hutakiwi kuyaruhusu kabisa yatawale maisha yako. Unaporuhusu mambo haya yakatawala maisha yako kuna namna ambayo unakuwa una haribu maisha yako, kuwa makini na fanyia kazi.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.