Followers

Waziri Mbarawa akagua mradi wa maji wa bwawa katika Mto Rufiji




WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa ametembelea mradi mkubwa maji wa bwawa katika Mto Rufiji utakaoweza kusaidia matumizi ya maji kwenye kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge)

Mradi huo unaotekelezwa Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia  Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (DAWASA) na umeweza kugharimu kiasi cha Milioni 604.9 ukiwa ni muendelezo wa mradi mkubwa wa maji unaoendelea Kisarawe.

Akizungumza baada ya kutembelea maporomoko ya Mto Rufiji Prof Mbarawa amesema kuwa mradi huo wa maji utakuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita 209,000( laki mbili na elfu tisa) kwa ajili ya matumizi ya kambi ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler's Gorge).


Amesema, mradi huo wa maji utawasaidia wakandarasi kuwa na miundo mbinu wezeshi itakayowapatia maji muda wote wa matumizi yao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanusi mkubwa.

"Miundo mbinu wezeshi itawapa fursa wakandarasi wafabye kazi kwa ufanisi mkubwa sana kwa  sababu maji yatakuwa yanapatikana muda wote na kila siku na hili litasaidia katika kuhakikisha mradi wetu wa ujenzi wa bwawa la umeme kumalizika kwa muda ulipangwa,"amesema Prof Mbarawa.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.