WHO: Robo tatu ya watu duniani wako hatarini kuugua
Shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watu duniani wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa mabaya, kutokana na sababu ya kutotaka kujishughulisha na afya zao.
Utafiti uliofanywa na WHO na kuchapishwa katika jarida la kitabibu la Lancet Global Health, ambalo lilichambua data iliyotolewa na washiriki milioni mbililili.
Utafiti huo umebaini kuwa kuna jitihada kidogo imefanyika kati ya 2001 na 2016.shirika hilo la afya uimwenguni limeonya kuwa watu wasiofanya mazoezi ya kutosha wanakabiliwa na hatari kubwa ya kukumbwa na shambulio la moyo, ugonjwa wa kisukari aina ya pili na wengine hukabiliwa na saratani.
Shirika hilo limeendelea kutanabahisha kuwa asilimia arobaini ya wamarekani hawajishughulishi na afya zao na kwamba hali hii ni mbaya zaidi katika nchi ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia na Iraq.
No comments
Post a Comment