ALIKIBA KUCHEZA TIMU ISIYO NA KOCHA KOCHA.
Na Fedson Goodness.
Klabu ya coastal union ya jijini tanga inataraji kushuka dimbani hapo kesho tarehe 28, kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya klabu ya Alliance ya jijini mwanza kwenye uwanja wa Nyamagana.
Ally Kiba ambaye alisajiliwa kwenye klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja anataraji kuwepo kwenye mchezo wa kesho, lakini kinachoshangaza zaidi ni kwamba klabu ya Alliance haina kocha mkuu, wala kocha msaidizi, aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Mbwana Makata pamoja na kocha msaidizi wake Kessy Mziray waliondoka klabuni hapo yapata wiki sasa kutokana na kile walichodai kuingiliwa kimajukumu na mmiliki wa klabu hiyo ambaye pia ni Meya wa jiji la Mwanza, ndugu James Bwire.
Ally tangu asajiliwe na coastal union amekwisha cheza mechi mbili pekee na katika mechi hizo aliingia dakika za mwisho kabisa na mpaka sasa hajafanikiwa kufunga goli hata moja.
Watu wengi wanasema huwenda Ally Kiba amekuwa hachezi mara kwa mara kutokana na kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya costal union na pia kutokana na ubora wa timu wanazokutana nazo, lakini kwa Alliance huwenda akacheza kwa dakika zote kutokana na wepesi wa mchezo huo pamoja na maswahibu wanayopitia klabu ya Alliance
No comments
Post a Comment