Followers

EL CLASICO MBOVU KUWAHI KUTOKEA DUNIA


Na Fedson Goodness
Tarehe 28 ya mwezi wa 10 ni siku ambayo miamba miwili ya ligi kuu nchini Hispania  inakutana kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama LA LIGA, miamba hiyo ni Real Madrid kutoka jijini Madrid pamoja na Fc Barcelona kutoka katika jimbo la catalunia.
Mchezo huu unafahamika pia kwa jina la EL CLASICO na utachezwa kwenye dimba la nyumbani la Fc Barcelona linalofahamika kama Camp Nou, ikumbukwe kwa mara ya mwisho timu hizi zilikutana tarehe 6 ya mwezi wa tano mwaka huu kwenye dimba hilo hilo la Camp Noun na mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili.
El clasico ya oktoba 28 inatazamwa kama el clasico itakayo kosa mvuto kutokana na kukosekana kwa baadhi ya wachezaji muhimu ndani ya timu hizi tofauti na ilivyokuwa kwenye el clasico za michezo ya nyuma, tayari mchezo huu utawakosa washambuliaji wawili wenye historia ya soka kubwa duniani, Lionel Messi kwa upande wa Fc Barcelona pamoja na Christiano Ronaldo kwa upande wa Real Madrid.

Lionel Messi ambaye ndiye mfungaji bora wa michezo ya El Clasico akiwa na mabao 26, atakosekana kutokana na kuwa na majeraha ya mkono, wakati Christiano Ronaldo yeye hayupo tena kwenye klabu ya Real Madrid baada ya kuhamia kwenye klabu ya Juventus.
Ukiachana na Messi na Ronaldo wachezaji wengine watakaokosekana kwenye mchezo huo ni pamoja na mabeki wawili wa timu hizo, samwel Umtiti kwa upande wa Barcelona pamoja na Marcelo kwa upande wa Madrid, wote hao wanaukosa mchezo huo kutokana na kuwa na majeraha.
kukosekana kwa wachezaji hao muhimu kwenye mchezo huo kuna toa taswira isiyo na mvuto kwa mashabiki wa timu hizo, lakini uzuri wa michezo ya aina hii hutoa nafasi kwa wachezaji wengine kung’ara.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.