Mbunge Mavunde amwaga neema kwa mafundi cherehani wa Dodoma Mjini
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde amezindua Umoja wa mafundi Cherehani Dodoma (UMACHEDO) na kuahidi kuwasaidia mafundi hao upatikanaji wa mashine za kisasa na mafunzo katika kuelekea uanzishwaji wa kiwanda cha ushonaji.
Mavunde ambaye pia ameteuliwa kuwa Mlezi wa Umoja huo,ameahidi kuwapeleka kwenye mafunzo maalum wanachama wa UMACHEDO katika kiwanda cha Opensanit Tabata na EPZA Mabibo-Dar es salaam kwa lengo la kuongeza ujuzi katika tasnia ya ushonaji.
Aidha Mbunge Mavunde amewaunganisha mafundi hao na mifuko uwezeshwaji wananchi kiuchumi ambapo kwa sasa wameanza kukopeshwa chini ya mfuko wa dhamana wa Rais (PTF)
Akizungumza kwa niaba ya umoja huo,Mratibu wa UMACHEDO Ndg Christopher Mullemwah amemuahidi Mbunge Mavunde kufanikisha azma ya uanzishwaji kiwanda cha umoja na kumshukuru Mavunde kukubali kuwa mlezi pamoja na misaada mbalimbali aliyotoa kufanikisha uundwaji wa Umoja huo.
No comments
Post a Comment