Followers

MECHI 6 KUMUONDOA UJERUMAN

Na Fedson Goodness
Germany
Mabingwa wa kombe la dunia kwa mwaka 2014 ambao ni timu taifa ya Ujerumani inapita katika kipindi kigumu ambacho kinawafanya mashabiki wengi pamoja na baadhi ya viongozi wa shirikisho la soka nchini Ujerumani kutokuwa na furaha juu ya matokeo ya timu hiyo.
Mwaka 2014 Ujerumani ilitwaa ubingwa wa dunia  chini ya kocha Joachim Law ambaye pia aliisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa mabara kwa ngazi ya vilabu mwaka 2017 nchini urusi akiwa na kikosi chenye mabadiliko makubwa tofauti na kile kilichotwaa  ubingwa wa dunia mwaka 2014 nchini Brazil.
Baada ya kufanya vyema shirikisho la soka nchini Ujerumani liiamua kumuongezea kandarasi ya miaka minne ya kukifundisha kikosi hicho hadi mwaka 2022, lakini baada ya kuongezewa kandarasi  kibarua chake cha kwanza kilikuwa ni michuano ya kombe la dunia kwa mwaka 2018 nchini Urusi ambayo hakufanya vizuri na kuishia kwenye hatua ya makundi.
Lakini mambo yanazidi kuwa si shwari ndani ya kikosi hicho kwani ndani ya miezi mitano tangu mwezi wa sita kikosi hicho kimepoteza mechi sita mfululizo pasipo kushinda mechi hata moja, zifuatazo ni mechi sita ambazo Ujerumani imepoteza tangu mwezi wa sita, Ujerumani 0 - 1 Brazil, Austrial 2 - 1 Ujerumani, Ujerumani 0 - 1 mexico, Korea kusini  2-0 Ujerumani, Uholanzi  3 – 0 Ujeruman na Ufaransa 2 - Ujerumani.
Baada ya matokeo hayo shirikisho la soka nchini humo linamuangalia kocha Joachim Law kwa jicho la tatu huku baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo wakianza minong’ono ya kutaka kumvunjia mkataba kocha huyo ambaye pia ni muangalizi wa timu za taifa za vijana za nchi ya Ujerumani.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.