Bodi ya udhamini Simba chini ya Mo yafikia patamu
BODI ya Udhamini ya Simba Sports Club Limited iliyo chini ya mfadhili wao bilionea, Mohammed Dewji ‘MO’ ipo kwenye hatua za mwisho za kumtangaza Selemani Matola kuwa mbadala wa Mrundi, Masoud Djuma.
Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu bodi hiyo ilipokutana na uongozi mpya ulioingia madarakani wiki moja iliyopita baada ya kufanya uchaguzi wa wajumbe na mwenyekiti wao mpya ambaye ni Swedy Mkwabi.
Simba ipo njiani kumleta mbadala huyo wa Djuma baada ya kutokea kutoelewana kati yake na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Patrick Aussems kabla ya kusitishiwa mkataba wake na kurudi Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, zoezi la kumpata msaidizi wa Djuma lipo chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu (C.E.O) mpya wa klabu hiyo, Crescentius Magori na kocha Aussems ambao tayari wamekutana kujadiliana masuala ya usajili pamoja na kocha msaidizi.
No comments
Post a Comment