Makala: Ndoa ya Ruby kivutio kwa DC Jokate na ushujaa wa Whitney Houston
Kwa mikono miwili mwaka 2015 mashabiki wa Bongpo Fleva walimpokea kwa mikono miwili muimbaji Ruby kutoka Tanzania House of Talent (THT).
Ruby aliwashika mashabiki vilivyo kupitia wimbo wake uitwao Na Yule ambao uliandikwa na Barnaba.Toka hapo amekuwa akifanya vizuri licha ya changamoto mbalimbali ambazo alipitia kwenye muziki wake baada ya kuondoka kwenye Menejenti yake ya awali. Tuachane na hilo.
Kwa sasa Ruby ameachia video ya wimbo wake unaokwenda kwa jina la Ntade ambao ulitokoa miezi mitatu iliyopita. Video hiyo imekuja kujibu kuhusu zile stori zilizodai kuwa Ruby alifunga ndoa kimya kimya.
Utakumbuka September 13, 2018 Ruby alichapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuwachanganya mashabiki wake mara baada ya kuonekana akiwa amevalia vazi la Bibi harusi.
Muimbaji huyo mwenye sauti ya pekee alichapisha picha hiyo na kuandika; MAMBO HADHARANI.Kuanzia hapo maswali yakawa ni mengi pasipokuwa na majibu ila ujio wa video hiyo ameonyesha kuwa picha hiyo ilitokana na utengenezaji wa hiyo video.
Kwanini DC Jokate
Kuelekea mwishoni mwa September mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo alizindua harambee ya kuchangia Programu iliyoianzishwa kwa ajili ya kutokomeza Zero.
Program hiyo imelenga kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo kwa kuhakika wanafunzi wanakuwa na madarasa mazuri ya kusomea, vifaa na chakula. Programm hiyo ililenga kukusanya Tsh. Milioni 100 lakini kwa taarifa ya awali awaliweza kupata Tsh. Milioni 125.062.
Katika harakati za program hiyo DC Jokate alifanya mahojiano na Wasafi TV na kueleza moja nyimbo anazopenda ni Ntade ya Ruby.
"Ntade ya Ruby, beatuful song, Ruby ana sauti ambayo ni kama sauti ya kiungu, kama Whitney Houston unajua kuna kuimba lakini kuna mwingine anaimba kama anaongea na roho yako," alisema DC Jokate.
DC Jokate anaujua muziki kwani naye amefanya na amekuwa kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva kwa muda, hivyo kumlinganisha Ruby na Whitney Houston amempa heshima kubwa kwake.
Whitney Houston ni Nani?
Whitney Elizabeth Houston ni muimbaji mkubwa aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini Marekani, alizawaliwa August 1963 na alifariki mwaka 2012 kwa kile kilichoelezwa ni matumizi ya dawa za kulevya.
Moja ya nyimbo za Whitney Houston zilizofanya vizuri zaidi ni ule uitwao I Will Always Love You, kwa mara ya kwanza uliandikwa na kurekodiwa na Dolly Parton mwaka 1974.
Whitney Houston aliurudia mwaka 1992 na uliweza kushinda tuzo mbili za Grammy mwaka 1994 katika vipengele vya Record of the Year na Best Vocal Performance by Female.
Baada ya Whitney Houston kuurudia umekuwa best sell single of all time na pia ni best sell single of all time by woman. Alifariki mwaka 2012 akiwa na miaka 48, chazo cha kifo chake kinaelezwa ni matumizi yaliyopitiliza ya dawa za kulevya.
No comments
Post a Comment