Followers

Mambo yanayotufanya tushindwe kufanikiwa mapema

 

Kuna baadhi ya watu wanazitambua njaa zao  na wengine hawazitambui njaa zao za mafanikio. Njaa hizo za mafanikio  zinatofautiana baana ya mtu mmoja na mwingine. Nimesema ni baadhi ya watu wachache ndio watu ambao wanajishughulisha usiku na mchana ili kuangalia ni mbinu zipi wanaweza kuzitumia ili waweze kufanikiwa.  Lakini watu hao wenye njaa ya mafanikio, mambo yao wakati wa kuyasaka mafanikio huwa ni mateso ya hapa na pale.

Watu hawa huzunguka huku na huko ili kupata maisha bora. Watu hawa naweza nikawaona ni watu ambao huwa wana sura za huzuni zaidi ila furaha huchukua kwa kiwango kidogo sana katika maisha yao. wapo baadhi ya watu kutokana na njaa walinazo kila kazi yeyote yupo tayari kuifanya. Ila tatizo linakuja ni kwamba pindi apato fursa ya kufanya kazi wengi wao wanapweteka na kutoonesha njaa walizokuwa nazo mwanzo pindi wapatapo nafasi ya kufanya kazi. Hivyo katika makala ya leo nataka nikushirikishe kwa nini watu hao huwa hivo.

Hii ndio sababu kubwa kwa nini watu wengi hawatumii nafasi walizozipata kwa asilimia mia moja;

Kuridhika na Hali uliyonayo.

Tafiti zinaonesha ya kwamba asilia kubwa ya watu wakipata kile walichokuwa wanakihitaji hawakifanyi kwa asilimi mia moja. Hii ni kutokana mtu anaona kitu hicho ameshakipata hivyo hana haja tena na kuanza kuendelea kuongeza juhudi na ubunifu katika kitu au jambo Fulani. Kimsingi ni kwamba binadamu ni watu wa kulalamika sana nasema hivi ni kiwa namaana ya kwamba leo hii ukikutana na mtu ambaye hana ajira au hafanyi biashara ni mtu wa kulalamika sana, na asilimia kubwa la kundi hili wengi wao husema nikija kupata kazi au nikija kufanya biashara nitafanya vizuri ili kutumiza ndoto zangu. Ila tazizo maneno hayo hugeuka dakika chache akilipata jambo hilo hafanyi kama alivyoahidi mwanzoni wakati wa akilitafuta jambo hilo.

Mfano leo hii tunaona baadhi ya wasanii wa nyimbo wanapotea katika sanaa,  hii mara tu baada ya kutoa wimbo mmoja ambao utapendwa na watu wengi.  Tatizo kubwa wengi wao huwa wanaridhika na mapokeo ya wimbo huo na kupweteka na kujiona tayari wameshafanikiwa  na mwisho wa siku hatuwasikii tena. Tatizo lao kubwa ni kuridhika na walichokipata mwanzo. Pia wengi wanasahau kujipanga upya na kuja kufanya vizuri katika kazi zake zote zianzokuja.

Tupo baadhi ya wafanyabahara huwa tunaridhika na kuona kile tunachokipata kama ni faida kubwa. Jambo la msingi na la kuzingatia ni kwamba hicho ulichonanacho usiridhike nacho  na kujiona wewe ni mkamilifu na kinatosha, la hasha bali jione una mapungufu kwa kuzitambua njia mbalimbali za kuweza kuongeza thamani katika biashara na kazi zingine unazofanya.

Tukumbuke ya kwamba ili kuyaona mafaniko katika kila shughuli ambazo tunanazifanya ni kwamba tujione ya kwamba vitu hivyo vinatudai kwa maana ya kwamba tusidhike na kuona vinatosha hapo vilipo. Leo hii mtu aliyegundua ndege haridhiki na ndege amabayo ameigundua bali anafikiria kitu kingine ambacho atakiongeza katika ndege ili kuongeza ubora au anafikiri kitu kingine zaidi ya ndege.

Kama ndivyo hivyo hata wewe katika jambo lolote ambalo unalifanya lazima ufikirie hivyo. Usiridhike na ulichonacho bali fikiria ni nini unakihitaji zaiidi ili kuongeza thamaani katika jambo ambalo unalifanya. Kuwa mtu ambaye ni mbunifu ambaye utatofautina na wengine.  Endapo utayafanya hayo kwa njia tofauti na zile ambazo umezizoea utakuwa tofauti sana na watu wengine na ndoto zako zitazidi kungara mara dufu.

Daima tukumbuke ya kwamba wewe ndiye mmiliki wa mafanikio yako, hivyo una uwezo mkubwa wa kuyafanya mafanikio hayo yakuwe au yafe. Kitu cha msingi ili kukuza biashara  au jambo lolote  ni kuamua tu na kuvifanya mambo kwa njia na tofauti ulizozioa .

Makala imeandikwa na; Benson chonya

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.