Rais wa Zanzibar asema ipo tayari kuimarisha ushirikiano uliopo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema Zanzibar ipo tayari kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizo.
Amesema hayo jana katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Intercontinental, wakati alipokutana na Jumuiya ya Magavana wa Kaunti za ukanda wa Pwani ya Kenya.
Lengo la mkutano huo nikujadili mambo mbali yenye mnasaba na maisha na shughuli za watu wa ukanda wa pwani, ambapo changamoto mbali mbali zinazozorotesha shughuli za kiuchumi zilijadiliwa.
Katika kikao hicho Dk.Shein alitoa fursa kwa kila mmoja wa Gavana wa kaunti hizo kuelezea mambo ambayo angependa kuelezea katika kikao hicho kwa kuzingatia malengo ya mkutano huo. Vile vile, alitoa fursa kwa viongozi wa Zanzibar aliokuwa amefuatana nao kutoa ufafanuzi na maelezo ya ziada kwa kuzingatia hoja zilitolewa na magavana wa akaunti hizo.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni haja ya kumarisha uhusiano baina ya Watu wa Zanzibar na watu Ukanda wa Pwani pamoja na watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa Kenya, pia pande mbili hizo, zilijadili njia bora za kuimarisha sekta ya uvuvi ambayo ni shughuli muhimu ya kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Viongozi hao walijadili juu ya umuhimu wa kukaa pamoja ili kuzifanyia kazi changamoto ziliiyopo zikiwemo za kukamatwa wavuvi wadogo wadogo wa pande zote mbili wenye kuvua katika mipaka ya Jamhuri ya Kenya na Tanzania.
No comments
Post a Comment