Followers

Jinsi ya kufanikiwa kimaisha zaidi ya hapo ulipo sasa


Ili uweze kuyafurahia maisha hayo ni vyema uweze kutambua mambo ya msingi yatakayokusadia kuweza kupiga hatua za kuelekea katika mafanikio.

Na miongoni mwa vitu vitakavyokusaidia kupiga hatua hizo za kimafanikio na hatimaye kufanikiwa zaidi ya hapo ulipo sasa unatakiwa kuweka vipaumbele vitakavyokusadia kuweza kufika mbali zaidi katika suala la mafanikio.

Watu wengi wanashindwa kupiga hatua za kimafanikio kwa sababu watu hao wanashindwa kuwa na vipaumbele vinavyowaongoza wao katika kufanya mambo yale ya msingi.

Kwa mfano utakuta mtu anataka kufanya kila jambo ambalo analiona linafaa mbele ya macho yake, kitendo hiki ndicho kitendo tunachoita kukosa vipaumbele,  na kuendelea kufanya hivi unaweza ukaona upo sawa kabisa kumbe unajipoteza mwenyewe pasipo wewe kujua.

Hivyo kila wakati unatakiwa kukumbuka ya kwamba  kwenye maisha ili uweze kufurahia maisha haya hatimaye kufanikiwa, unatakiwa kuhakikisha unakuwa ni mtu unayeongozwa na vipaumbele katika kutenda yale yaliyo ya msingi. Yaani ni lazima uwe na ratiba inayokuongoza wewe katika kufanya mambo yako, kwa kuzingatia kipi cha kufanya na kipi si cha kufanya, kwani ukifanya kila kitu utakuwa hauna vipaumbele.

Hivyo kila wakati unatakiwa kukumbuka ya kwamba ili uweze kufanikiwa katika maisha yako unatakiwa kupanga na kuongozwa na vipaumbele ambavyo vitakufanya uweze kusonga mbele katika suala la kupata mafanikio unayoyataraji.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada nikutakie siku njema na mafanikio mema endelea kutembelea Supernida blog kila wakati.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.