Followers

KAA MBALI NA SIMBA WEWE,HUYO CHAMA SIO WA AFRIKA HII,WAIFUMUA BILA HURUMA NKANA.

 NA KAROLI VINSENT 

Ama kweli Simba ndio wa kimataifa ,ndivyo walichokionesha leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuichabanga  bila huruma timu ya Nkana kutoka Zambia kwa  Mabao 3-1    kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na kutinga hatua ya Makundi. 

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha mwenye “Fomisheni” ya hatari Mbelgiji ,Patrick Aussems,ambapo Dakika 5 za mwanzo  walianza vizuri ila ndani ya dakika 15 walipoteana na kuruhusu bao la dakika ya 16 lililofungwa na Walter Bwalya baada ya kushambulia lango la Simba kwa muda mrefu. 

Katika Mchezo huo uliojaa na mashabiki wengi wa Simba Iliwalazimu  wasubiri mpaka dakika ya 29  kuwasazisha Gori hilo ambalo lilofungwa na Kiungo,Jonas Mkude,akimalizia pasi ya Claytous Chama ambaye alionyesha kiwango cha hatari katika mchezo huo  na kuufanya mechi kuwa bao moja kwa moja.

Mambo yakazidi kuwa mazuri zaidi kwa Mabingwa hao wa Ligi kuu Tanzania bara ambapo kwenye dakika ya 45  Mshambuliaji  wao hatari zaidi na wakuogopwa,Meddie Kagere ,aliandika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya  James Kotei.

Kipindi cha pili dakika ya 88  Claytous Chama alifunga bao akimalizia pasi ya Hassan Dilunga ambaye aliingia sabu .

Simba wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3.

Ambapo sasa wanasubilia Ratiba ya Makundi ambayo mda wowote kutoka sasa itapangwa,endelea kufuatia Mtandao wa Supernida.com kujua simba wamepangiwa na timu gani kwenye hatua ya makundi.

Katika Mchezo huo uliojaa na mashabiki wengi wa Simba Iliwalazimu  wasubiri mpaka dakika ya 29  kuwasazisha Gori hilo ambalo lilofungwa na Kiungo,Jonas Mkude,akimalizia pasi ya Claytous Chama ambaye alionyesha kiwango cha hatari katika mchezo huo  na kuufanya mechi kuwa bao moja kwa moja.
 Mambo yakazidi kuwa mazuri zaidi kwa Mabingwa hao wa Ligi kuu Tanzania bara ambapo kwenye dakika ya 45  Mshambuliaji  wao hatari zaidi na wakuogopwa,Meddie Kagere ,aliandika bao kwa kichwa akimalizia pasi ya  James Kotei.
Kipindi cha pili dakika ya 88  Claytous Chama alifunga bao akimalizia pasi ya Hassan Dilunga ambaye aliingia sabu .
Simba wanafanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3.
Ambapo sasa wanasubilia Ratiba ya Makundi ambayo mda wowote kutoka sasa itapangwa,endelea kufuatia Mtandao wa DarMpya.com kujua simba wamepangiwa na timu gani kwenye hatua ya makundi.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.