Mahakama ya vileo yasema haitatoa vibali kwa baa ambazo hazitafuata masharti
Na.Thabit Madai,Zanzibar.
Mahakama ya vileo Zanzibar imesema haitatoa vibali vipya kwa mwaka 2019 kwa Baa ambazo hazita fuata masharti yaliyowekwa pamoja na kuzifungia baa ambazo zimekuwa zililalamikiwa na wanachi kwa kuendesha biashara ya pombe kiholele.
Aidha imewataka wanachi kuweza kuendelea kutoa taarifa kwa baa ambazo zimeanzishwa kinyume na utaratibu pamoja na zile ambazo zimekuwa hazifuati masharti ya biashara hiyo.
“hatuta waachia wale wote ambao wamekuwa wakiendesha biashara za mabaa pamoja na vileo kinyume na taratibu zilizowekwa”ilisema mahakama ya vileo.
Akizungumza na waandishi wa habari Nje ya mahakama ya Mfenesini katibu wa Mahakama hiyo Saleh Abdallah alisema hatua hizo zimekuja mara baada ya mahakama mbali mbali nchini kuanza kusikiliza maombi ya vibali kwa wafanya biashara wa baa.
Alisema mara baada ya kusikiliza maombi kwa wafanya biashara hao watafuatilia kwa kuona wamefuata vigezo na masharti ya kuanzisha biashara hiyo huku ikizingatia malamiko yanayotolewa na wananchi juu ya biashara ya baa na pombe.
Aidha alimeahidi kutotoa vibali kwa kwa baa zinazotoleta usumbufu kwa wananchi hasa karibu na maakazi ya wanachi, nyumba za ibada na zenye kukiuka maadili ya vileo.
Hata hivyo alisema wakati bodi ya vileo ilipofanya ukaguzi kwenye maeneo yanayouza biashara ya pombe ilikagua na kugundua matatizo mbalimbali ikiwemo uchafu wa mazingira na mambo mengine kama upigwaji wa miziki.
Kwa upande mwingine Saleh aliwasisitiza wananchi kujitokeza kuweka pigamizi zao kwa baa zinazowasababishia matatizo ili mahakama iweze kuzifutia vibali au hata kuzifungia kabisa baa hizo kwani nguvu ya mahakama inakuja baada ya kuwepo mashirikiano ya wananchi.
Amezitaja jumla ya baa 31 zilizoomba vibali kwa ajili ya kukata lessen ya kuuzia pombe katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja ambazo hata moja haikupata mpingaji ambapo hali hiyo itawapa fursa wamiliki na wawekezaji wa biashara hiyo kuendelea kupata mwanya wa kuuza pombe kila siku kukicha.
Aidha alisema wananchi wanahaki ya kuzipinga baa kwa mujibu wa sheria ya vileo Zanzibar hivyo wasiwe na wasiwasi juu ya hilo badala yake kushiriki ili kupata haki zao za msingi.
Download App hii kupitia link kwa kubonyeza https://play.google.com/store/apps/details?id=com.supernida.blog uweze kupata updates zote kwa ulahisi zaidi
No comments
Post a Comment