Followers

Mmiliki kampuni ya mabasi ya Muro akwepa kifungo cha miaka minne.



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kumuhukumu mmiliki wa Kampuni ya Mabasi ya Muro, Majid Kimaro kulipa faini ya Shilingi Milioni 115 au kifungo cha miaka nane jela baada ya kukiri kosa la utakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu amekikwepa kifungo hicho kwa kulipa faini fedha hiyo.

Muro anadaiwa aliongoza genge hilo la uhalifu ili kuiba mafuta katika bomba linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Pia Mahakama imeamuru gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 856 ADH ambalo lilitumika kuiba mafuta zaidi ya lita 26,875.25 za Dizeli na Petroli litaifishwe na kuwa mali ya serikali.

Asante kwa kuendelea kutufuatilia 
Supernida inapenda kukutakia heri ya Christmas na mwaka Mpya kwa 
Comment yako na kwa ushauri wowote Karibu danielothmary@gmail.com/0767673288

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.