Tafakari muhimu ya maisha kabla ya kumaliza mwaka 2018.
Tunayo kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutupigania mpaka dakika hii tunapoendelea kutumia hewa ya oksjeni pasipo hata kulipia hata shilingi moja. Tunaamini Mungu wetu ni mwema na mwanifu pia kwani kila wakati yu pamoja nasi, hivyo tunamuomba atufanikishe tuweze kuuvuka salama mwaka huu na kuanza mwaka mpya salama.
Ndugu msomaji wa makala haya kupitia Muungwana blog hebu tuzame katika fikra zetu kisha tutafakari juu ya maisha ambayo tuliyaashi mwaka 2018 kama ifutavyo:
Tuwaze Kuhusu malengo yetu.
Je yale malengo ambayo tuliyapanga yamekamilika kwa asilimia ngapi? Kama tumekwama kuyakamilisha ni wapi ambapo tulikosea?
Tuwaze kuhusu maisha ya kawaida.
Je tuliIshi maisha ya aina gani? Ni maisha ya kuwa vikwazo kwa wengine au ni maisha ya kuwafurahisha wengine?
Maisha Mahusinao na Mwenyezi Mungu.
Vipi kuhusu mahusiano yetu na Mungu wetu, je yalikuwa na maisha yenye kutenda yaliyo mema au yalikuwa ni maisha ya kumkwanza Mungu kwa kuendelea kutenda dhambi kila wakati?
Kuhusu kuwajali watu wengine.
Ndugu mwaka 2018 ulikuwa ni mwaka wa aina gani kwako kuhusu kuwasaidia watu wenye matatizo na shida mbalimbali?
Maisha kuhusu mahusiano yako na familia yako.
Miasha juu ya familia yako yalikuwaje? Au uliwa bize na mambo yako bianafsi kuliko kuwa na familia yako.
Maisha juu matumizi ya pesa kiujumla
Endelea kutafakari, Hivi mwaka 2018 uliwa ni mwaka wa aina gani kwako juu ya matumizi yako ya pesa, je yalikuwa ni matumizi ya kawaida au ni matumzi ya kuponda mali kufa kwaja.
Naomba wakati unatafakari mambo haya chukua kalamu na karatasi kisha andika kila kitu pasipo kuona aibu maana kanuni hii ni kanuni muhimu ya kutafakari ili kujua mwaka 2018 ulikuwa ni mtu wa aina gani ili uweze kufanya marekebisho kwa mwaka ujao yaani mwaka 2019.
Yamkini yapo mambo mengi uliyapanga kuyafanya na ado haujayafanya ila naomba nikwambie umeshindwa kufanya mambo uliyoyafanya kwa sababu kuna Tofauti kubwa kati ya Mawazo na Ndoto, ukiona ulipanga kufanya jambo fulani mpaka dakika hii hujachukua hatua yeyote ile, basi ujue fika haikuwa ni ndoto bali yalikuwa ni mawazo tu, kwani mara zote ni heri kuyabadili mawazo yawe katika ndoto, huku utekezaji wa ndoto hiyo ukiaanza mara moja. Kama ni mawazo kila mmoja anayo lakini wanachukua hatua ni wachache,
Hivyo nakusihi kuwa mwaka 2019 ili uwe ni mwaka wenye neema na mafanikio kwako kwa kila jambo, unatakiwa ujifunze kuchukua hatua stahiki za kiutendaji kwa kile unachokiona ni bora zaidi kwako.
Na: Benson Chonya
No comments
Post a Comment