Ufahamu ugonjwa wa Gumboro ( Infectious Bursal Diseases) katika ufugaji wa kuku.
Ni ugonjwa wa utokanao na virusi viitwavyo ”BIRNAVIRUS" . Ugonjwa huu huwashambulia kuku na ndege wengine wafugwao.
Kuenea/kusambaa kwa ugonjwa.
Kutoka banda moja kwenda linginge.
Kupitia kinyesi kinyesi cha kuku anayeumwa.
Dalili za Ugonjwa
Kuku hutapika na kuharisha majimaji.
Manyoya husimama.
Kuku husinzia na kukosa hamu ya kula.
Vifo hufikia hadi asilimia thelathini (30%).
Kuku hujidokoadokoa sehemu ya haja kubwa.
Cloaca huvimba.
Chini ya ngozi hasa mapajani vidonda hutokea hasa vifaranga.
Namna ya kukinga na kuzuia ugonjwa wa Gumboro
Safisha banda kwa dawa za kuua vijidudu (Disinfectants).
Wapatie chanjo ya Gumboro vifaranga wakiwa na umri wa wiki 2 na rudia tena wakiwa na umri wa wiki 3 (yaan siku ya 14 na 21)
Tiba za ugonjwa wa Gumboro
Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila kwa msaada zaidi wasiliana na mtaalam au daktari wa mifugo. Asante
Asante kwa kuendelea kutufuatilia
Supernida inapenda kukutakia heri ya Christmas na mwaka Mpya kwa
Comment yako na kwa ushauri wowote Karibu danielothmary@gmail.com/0767673288
No comments
Post a Comment