Wachezaji wanne Simba kutolewa kwa mkopo
Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza kuwapeleka kwa mkopo wachezaji wake wanne ili kuimarisha zaidi viwango vyao baada ya kukosa namba kwenye kikosi.
Simba imefikia maamuzi hayo ili kuwapa nafasi ya kuonesha uwezo wao vizuri na baada ya huduma yao kumalizika watarejea kama kawa lindoni kuendelea na kazi.
"Tumewapeleka kwa mkopo wachezaji wetu wanne katika klabu kadhaa na wachezaji hao ni Marcel Kaheza - AFC Leopards ya Kenya, Mohammed Rashid - KMC, Said Nduda - Ndanda FC na Salum Juma Ishaka wa under 20 anaekwenda Ashanti FC ya Ilala.
"Pia kama mnavyojua Simba imesajili mchezaji mmoja tu katika dirisha dogo ambae ni Zane ‘CAFU' Coulibaly raia wa Burkina Faso toka klabu ya Asec ya Ivory" Patrick Aussems.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara hivi sasa wapo katika mawindo ya kucheza na Nkana Red Devils katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Jumapili ya wiki hii watacheza kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
No comments
Post a Comment