HISTORIA FUPI YA RAIS MPYA WA DRC CONGO FELIX TSHISEKEDI TSHILOMBO
Pichani. Felix Tshisekedi Tshilombo ndie Rais Kwa sasa
ByAnaitwa Felix Antoine Tshiseked Tshilombo alizaliwa tar.13/Juni/1963 mji wa (Leopoldville) sasa Kinshasa.
Ni Kiongozi wa chama kikuu na kongwe cha upinzani kiitwacho Union for Democracy and social progress nchini Congo
January 9,2019 ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais nchini Congo.
Baba yake ni Etienne Tshisekedi ,ambaye ndio muasisi wa chama pinzani cha UDPS ambacho ndio mtoto wake Felix sasa ndio kiongozi leo.
Baba yake aliunda chama hicho pinzani cha UDPS mwaka 1980's alipokuwa anampinga Kiongozi Mobutu Sese Seko Kuku Ngebendu wa Zanga (Kiongozi aliye muondoa Patrice Lumumba 1961) kumbuka Mobutu jina lake ni Joseph ila alikataa kujiita majina ya kizungu,na 1971 alibadilisha jina la Congo kuwa Zaire na jina lake Joseph kuwa Mobutu 1972.
Baba yake Felix ,muasisi wa chama cha UDPS ndio alikuwa mpinzani mkubwa wa Mobutu .Baadaye Baba yake Felix ,Etienne Tshisekedi aliwekwa kizuizini kijijini kwao Kasai.Na Felix aliondolewa shuleni akapelekwa Kasai kwa baba yake kizuizini .
1985 Mobutu akawaruhusu Mama wa Felix ,na ndugu zake wengine kuondoka Kasai wakaenda ishi Ubeligiji ambapo alisoma na kupata kazi. Alisomea Bussines and marketing
Alipokuwa ubeligiji aliendelea kushiriki siasa na akateuliwa kuwa Kiongozi wa mambo ya nje na mahusiano ya chama based in Brussels ubelgiji mwaka 2008.
Alitengeneza marafiki wengi na wakubwa akiwa nje.
2011 alipata kiti bungeni kuwa mbunge akiwakilisha mji wa Mbuji Mayi , Kasai (kwao),ila sababu hakuwepo kiti chake kilibatilishwa baadaye( invalidated for absenteeism).
May ,2013 aliteuliwa kama rapporteur katika Tume ya uchaguzi wa Congo (CENI-Independent National Electrol Commission,alikataa akasema "sheria inakataa kiongozi yeyote ndani ya Tume kuwa mwanachama mimi ni mwanachama wa chama".
Octoba 2016 bado akiwa nje ubeligiji aliteuliwa kuwa naibu katibu mkuu wa chama chao UDPS ,Mwaka 2017 February 1 Baba yake muasisi wa chama cha UDPS Etienne Tshisekedi akiwa ubeligiji alifariki akiwa na miaka 84.
Mwaka huo huo 2017 ,Felix alirejea nchini Kongo akitokea ubelgiji katika uwanja wa Ndjili jumapili.Siku hiyo kulikuwa na maandamano makubwa ya kumpokea viongozi watatu wa upinzani walikamatwa .
Mwaka jana 2018 mwezi march 31 aliteuliwa kuwa Kiongozi mkuu wa Chama cha UDPS baada ya kifo cha Baba yake na wakamteua kama mgombea wa Urais wa chama cha UDPS . katika uchaguzi huu uliofanyika.
Januari 9/ 2019 ametangazwa kama mshindi wa kiti cha Urais DRC-Congo kwa kura zaidi ya mil 7 au 38.6% dhidi ya Martin Fayulu aliyepata kura mil. 6.4 mpinzani pia , Emmanuel Shadary aliyepata kura mil.4.4 anayependwa na kabila.
Asanteni kwa kuendelea kutufuatilia hapa supernida blogs endelea kuwa Nasi.
Shukran.
No comments
Post a Comment