Followers

Kigogo Yanga aitaka Serikali kuingilia kati suala la Uchaguzi



Mbaraka Igangula ambaye ni Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti katika klabu ya Yanga ameitaka serikali kuweka mkono wake katika uchaguzi ambaoulipaswa kufanyika Januari 13 2018.

Igangula amefunguka kuitaka serikali iingilie kati akiamini kuna baadhi ya watu wamefanya maamuzi hayo kwa sababu zao binafsi na baadhi ya wanachama kusababisha mahakama izuie uchaguzi huo baada ya kufungua kesi wakidai kuna sintofahamu imejitokeza.

Ameongeza kuwa Yanga imekuwa na makundi mawili ambapo moja alieleza linataka uchaguzi ufanyike na lingine likipinga usifanyike.

Kitendo hicho kimemkera Igangula ambaye anahitaji serikali ijaribu kuchunguza suala hilo pengine inawezekana kuna namna imefanyika.

Mahaka ilizuia uchaguzi wa Yanga ambapo sasa utapangiwa tarehe nyingine endapo mahakama itafikia maamuzi ya kuuruhusu ufanyike.

Download App hii kupitia link kwa kubonyeza https://play.google.com/store/apps/details?id=com.supernida.blog uweze kupata updates zote kwa ulahisi zaidi.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.