Mambo yatakayokusaidia kuweza kuishi ndoto zako
Kila mmoja ana ndoto zake katika maisha yake. Wengine wana ndoto kubwa za kubadilisha ulimwengu huu, huku wengine wakiwa na ndoto za kuishi maisha ya kupata mahitaji yao ya msingi tu.
Wote hawa wanahitaji kuzitimiza ndoto zao; lakini kuna vikwazo na mambo mbalimbali ambayo huwazuia watu wasiishi ndoto zao na kuishia kulamu na kulalamika hasa uzeeni.
Fuatana nami katika makala hii nikueleze dondoo za msingi zitakazokuwezesha kuishi ndoto zako.
Tathimini upya marafiki zako
Kila mtu ana marafiki katika maisha yake, lakini si wote wana manufaa kwako. Je ulishawahi kujiuliza ni marafiki wangapi uliokuwa nao shule ya msingi au sekondari na bado wanakufaa hadi sasa? Marafiki wanatakiwa wakuinue unapoanguka au unapozama wakuokoe na si kukuzamisha zaidi.
Je ni marafiki gani wa kuwaepuka?
Marafiki wasiojali muda na wavivu.
Marafiki wanopenda starehe na anasa.
Marafiki wasiopenda elimu na maarifa.
Marafiki wasiokuwa na malengo na maono ya mbeleni.
Marafiki wasiojua kuweka akiba – wao hutumia kila wanachokipata.
Marafiki wasioweza wala kupenda kukushauri na kushauriwa.
Ukiwaepuka hawa hakika utabakia na wale ambao hawatakuwa ni kikwazo kwako wewe kutimiza na kuishi ndoto zako.
Jikite kwenye ratiba ya mafanikio
Tuna mambo mengi sana ya kufanya humu duniani, lakini siyo yote hutuwewezesha kutimiza ndoto zetu. Hakikisha unapanga ratiba yako kwa kuhakikisha unaongeza maarifa na unafanya kitu chochote kwa siku ili kufikia au kutimiza ndoto zako.
Mambo ya kuzingatia katika hili:
Tumia muda vyema (Epuka vitu vinavyopoteza muda kama vile facebook, Televisheni n.k).
Jifunze kitu kipya kila siku, pia soma vitabu na makala mbalimbali kama hii unayoisoma.
Sogeza hatua moja kila siku kuelekea malengo yako.
Weka akiba.
Linda afya yako (kwa mazoezi, tabia njema na lishe bora).
Tafuta muda wa kupumzika na kuburudika
Kwa kuwa unatafuta kuishi ndoto zako, haimaanishi hauhitaji kupumzika au kuburudika. Unapopumzika unaupa mwili na ubongo wako nafasi ya kuwa katika hali nzuri zaidi ili uweze kufanya kazi kwa ubora zaidi.
Kwa mfano kama unapenda piano unaweza kupiga piano au ukaenda kutazama mandhari ya asili kama vile milima na wanyama. Kumbuka epuka starehe na anasa zisizokuwa na maana kama vile pombe na uzinzi.
Hapa nimeeleza dondoo ambazo zitakuwezesha kuishi ndoto zako kama utazitilia maanani. Nakusisitiza kuwa wakili mzuri wa muda pamoja na rasilimali ulizonazo kama vile fedha. Jiwekee malengo na uyafuate katika maisha yako.
Download App hii kupitia link kwa kubonyeza https://play.google.com/store/apps/details?id=com.supernida.blog uweze kupata updates zote kwa ulahisi zaidi.
No comments
Post a Comment