Mtoto wa miaka minne abakwa akiwa shuleni
Jeshi la polisi jijini Kisumu nchini Kenya linachunguza tukio la kubakwa kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne akiwa shuleni.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, mama wa mtoto huyo alitoa taarifa akieleza kuwa mtoto wake huyo anayesoma shule ya awali alianza kulalamika kuwa anasikia maumivu alipokuwa akimuogesha baada ya kutoka shuleni.
Mama huyo alisema kuwa baada ya kumbana mwanaye, alimueleza kuwa mtuhumiwa alimtishia na kumtaka asimwambie mtu yeyote kuhusu kitendo alichomfanyia akiwa katika mazingira ya shule ambayo iko ndani ya eneo la Kanisa, kando ya barabara la Kisumu-Nairobi.
Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Jaramogi Oginga Odinga, alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani siku iliyofuata. Polisi wameelza kuwa vipimo vya daktari vilionesha kuwa mtoto huyo aliingiliwa katika sehemu zake za siri.
Kwa mujibu wa Citizen ya Kenya, katika jitihada za kumtia nguvuni mtuhumiwa, wazazi wa mtoto huyo jana (Alhamisi) walifanya kikao na uongozi wa shule.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa baada ya kikao hicho hawakutaka kuzungumza na waandishi wa habari.
Kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani, watoto wengi wamekuwa wakibakwa na kunyanyaswa kingongo na jamii hususan watu wao.
Ripoti ya utafiti uliofanywa na Sara Jerop Ruto wa Chuo Kikuu cha Kenyatta na kuchapishwa kwenye Jarida la ‘International Coorporation in Education’, imeeleza kuwa kati ya watoto 1,206 waliohojiwa kama waliwahi kulazimishwa kufanya mapenzi, jumla ya watoto 310 (wasichana 198 na wavulana 112) walikubali kuwa waliwahi kufanyiwa hivyo.
No comments
Post a Comment