Naibu Waziri atoa wito kwa wadau mbalimbali kuwasaidia wenye ulemavu
Wito umetolewa kwa wadau binafsi, Makampuni na Mashirika mbalimbali kuwasaidia watu wenye ulemavu ili kukidhi mahitaji yao ikiwemo kuwaendeleza katika shughuli na vipaji vyao.
Witohuo umetolewa na Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi ,Vijana, Ajira na wenyeulemavu Stella Ikupa,alipokuwa akikabidhi Bajaji kwa Mama Leonea Leonard ambaye ni mlemavu wa miguu ,ambapo amesema Bajaji hiyo ameipata kwakushirikiana na mdau baada ya kumweleza kuhusu shida ya Mama huyo.
“Wahitaji wako wengi Tanzania ,unaweza kumsaidia Mama leo au unaweza kumsaidia mhitaji mwingine, leo tumempatia Bajaji inaweza kumsaidia katika shughulizake lakini pia bado analo hitaji lakusaidiwa kurecord nyimbo zake tunaomba mdau mwingine aweze kujitokeza amsaidie aweze kurecord ‘’Alisema Ikupa
Kwa upande wake Mama Leonea Leonard amemshukuru Mhe. Stella Ikupa, kwa moyo wake wa kujali watu bila kujali kuwa ni ndugu yake ama kuwa anaulemavu bali anasaidia watu wote, amesema watu wengi wanauwezo kifedha lakini hawana moyo wa kusaidia, Bajaji hii angeweza kuitumia kwa mambo yake mengine lakini kaamuamua kumpatia yeye hivyo amemshukuru Mungu kwa Upendo huo.
"Stella Ikupa, Joshua na Mke wake kwapamoja nawashukuru sana Mungu awabariki Kwa kunisaidia Bajaji hii sina cha kusema sana zaidi ya kuwashukuru na kuwaombea Mungu awainue mzidi
kufanikiwa ,Bajaji hiimimi itanisaidia sana sina mahali pa kuishi naweza kukusanya kidokidogo nami niwe na makazi yangu na pia nahitaji sana kurecord nyimbo zangu”Alisema.
Mama Leonia amesema yeye hakuzaliwa na ulemavu bali alipata ajali ya gari miaka minane iliyopita, ambapo katika ajali hiyo walikufa watu kumi nakupona wawili akiwemo yeye,pia ameelezakuwa yeye ni fudi kushona nguo ila hana mashine na anakipaji cha kuimba nyimbo.
No comments
Post a Comment