Rais Magufuli ampa pole Rais Kenyatta shambulio la Ugaidi Kenya.
Rais wa Jahmhuri ya Muungwano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za pole Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kufuatia shambulio la ugaidi lilotokea nchini humo.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter Rais Magufuli ameeleza kuwa alizungumza na Rais Kenyatta na kumpa pole.,
"Punde nimezungumza na Mhe. Kenyatta kuhusu shambulizi la Jijini Nairob.Pole sana Mhe. Rais na pole sa na wananchi wa Kenya.Tupo nanyi katika kipindi hiki cha majonzi. Nawaombea Marehemu wote walale mahali pema peponi, Amina," alieleza Rais Magufuli
Hadi sasa idadi ya watu waliofariki katika shambulio la wanamgambo wa Somalia, walipoivamia hoteli moja mjini Nairobi imeongezeka hadi 21 kwa mujibu wa serikali.
No comments
Post a Comment