Sheria za kuweka watu ndani mnazo lakini msizitumie vibaya - Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema amewaeleza Wakuwa wa Wilaya kuwa wanamamlaka makubwa kisheria lakini isiwe sababu ya kuyatumia vibaya.
Ameyasema hayo leo Ikulu Dar es Salaama wakati akiwaapisha Majaji sita wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama Kuu.
"Sheria za kuweka watu ndani mnazo lakini msizitumie vibaya, mtu anawekwa ndani halafu
baadae mnamtoa heti amejifunza bila hata haumjampeleka mahakamani is not fair," amesema.
Ameendelea kwa kusema, 'Wakuu wa Wilaya mna mamlaka yenu lakini myatumie
vizuri, ni kweli sheria imewapa mamlaka lakini ni muhimu kuyatumia vizuri mamlaka yenu, bahati
nzuri hili limeshasemwa sana na watu wengi nami narudia, Wakuu wa Wilaya mtumie mamlaka yenu vizuri" amesema Rais Magufuli.
No comments
Post a Comment