Ujue wimbo unaotajwa kuwa bora kwa mazoezi kutoka kwa Eminem
Wimbo wa msanii Eminem kutokea Marekani uitwao Till I Collapse umetajwa na mtandao wa Spotify kuwa wimbo bora wa mazoezi (workout song) kwa muda wote duniani.
wimbo ambao aliuachia mwaka 2002 ambapo Eminem alimshirikisha Nate Dogg, umeongozwa kwa kuchaguliwa na kusikilizwa na watu wengi kwa muda wote ukifuatiwa na 'Lose Yourself' ambao ni wa kwake pia.
Namba tatu na nne zimekamata na Kanye West kupitia nyimbo zake, Stronger na Power, huku namba tano ikienda kwa Macklemore kupitia wimbo wake uitwao Can't Hold Us ambao amemshirikisha Ryan Lewis.
No comments
Post a Comment