Usipokula matunda unakosa faida hizi mwilini
Matunda yana faida nyingi sana za kiafya mwilini. Ukiachana na ladha tamu inayotokana na kula matunda, kila mtu anashauriwa ale matunda tofauti yasiyopungua matano (5) kwa siku ili kupata faida zote mwilini. Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha kinga ya mwili, kupunguza sukari kwenye damu, kungarisha ngozi, kuleta nguvu na kuleta mafuta asilia kwenye mwili.
Watu wanaopendelea kula matunda na mboga za majani kama sehemu yao kubwa ya mlo wa kila siku hujenga kinga madhubuti za mwili dhidi ya magonjwa. Matunda yana virutubisho asilia ambavyo ni mahususi katika kujenga mwili na kuufanya kuwa na afya njema. Matunda hubeba virutubisho muhimu kama potasiam, vitamin C, vitamin A, nyuzi nyuzi (fiber) na folic acid.
Ulaji wa matunda unasaidia mwili hukufanya kupata faida zifuatazo:
Yanapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi
Yanakinga mwili dhidi ya aina za saratani
Nyuzi nyuzi (fiber) za kwenye baadhi ya matunda kama maembe zinasaidia kulinda dhidi ya magojwa kama mshituko wa moyo (heart attack), fetma na kisukari. Lakini pia inasaidia kupunguza madhara ya uvimbe unaotokana na kuwa na chumvi nyingi mwilini.
Kula matunda yenye potasiam kama ndizi na apricot kwa wingi yanasaidia kupunguza magonjwa ya shinikizo la damu. Matunda aina hizi husaidia pia kupunguza mawe kujaa kwenye figo.
Vitamin C ni muhimu katika mwili kwasababu inasaidia ukuaji na utengenezaji wa tishu za mwili. Mfano ni meno na fizi. Vitamic C inasaidia pia uchocheaji wa uponaji wa vidonda kwa haraka. Vitamin C inapatikana kwenye matunda mengi machachu, mfano machungwa, limao n.k
Folic acid inasaidia kutengeneza chembe hai nyekundu za damu mwilini. Wanawake wajawazito au walio kwenye umri wa uzazi wanashauriwa sana kula vyakula vyenye folic acid kwa wingi ili kusaidia ukuaji wa mototo tumboni na kudhibiti dhidi ya magonjwa.
Ni wazi kuwa huwezi kupata matunda ya aina yote kwa wakati mmoja, vilevile matunda mengi uanapatikana katika kipindi fulani za msimu wa mwaka. Matunda aina fulani kama sio msimu wake basi huwa yanuzwa kwa bei ya juu sanaa.
Hivyo inashauriwa kwa kipindi/msimu ambacho matunda fulani yanapatika, kula kula kwa wingi, tukihamia msimu mwingine na matunda mengine kula kwa wingi. Hi husaidia mwili kuwweka reserve mwilili hata ukikosa kipindi fulani lakini kuna madini akiba yaliyohifandhiwa mwilini.
Download App hii kupitia link kwa kubonyeza https://play.google.com/store/apps/details?id=com.supernida.blog uweze kupata updates zote kwa ulahisi zaidi.
No comments
Post a Comment