Yanga wataja sifa za Viongozi wanaofaa kuongoza Klabu yao
Uongozi wa Yanga umetaja sifa za Viongozi ambao wanapaswa wapewe nafasi ya kuongoza timu yao.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji na Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Siza Lyimo amesema kuwa kiongozi bora ni yule anayefuata misingi bora ya uongozi ikiwa ni pamoja na uadilifu.
"Kiongozi bora anajengwa na misingi ya uadilifu, hivyo huwezi kuongoza kama hauna hulka ya ujasiri na kuwa muungwana katika mambo ambayo unayafikiria ama kuyatenda.
"Wale ambao wana hulka za kuwadanganya wapiga kura kwa kutoa rushwa ili wachaguliwe wanajivua sifa za kuwa viongozi, ni wajibu wa wanachama kuchuja na kujua aina bora ambao tunahitaji waweze kutupa kile ambacho tunahitaji," alisema Lymo
Wanachama wa Yanga wanatarajiwa kufanya uchaguzi Januari 13, uchaguzi utakaofanyika katika ukumbi wa Polisi Messi Oystebay kuanzia saa moja kamili asubuhi na wanachama wenye kadi za benki pamoja na zile za kitabu ndio wanaruhisiwa kuchagua viongozi
No comments
Post a Comment