Ommy Dimpoz afunguka mazito aliyopitia Hospitalini
.
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesimulia mazito aliyopitia wakati alipokuwa akiumwa hadi sasa aliporejea kwenye hali yake ya kawaida.
Muimbaji huyo kwenye mahojiano na XXL ya Clouds FM amesema upasuaji wake wa awali ulichukua muda wa saa zaidi ya 10 na ulikuwa ni sehemu kubwa ya tumboni.
"Mara ya kwanza kufanyiwa upasuaji kabla sijafanyiwa madaktari waliniambia upasuaji unaoenda kufanyiwa ni mkubwa hivyo tunakupa muda wa kukaa na kujitafakari tena na nikaongea na familia yangu pamoja na wasimamizi wangu na wao waliniambia tunaimani utatoka salama," amesema.
Ameendelea kwa kusema, 'Nikafanya na upasuaji huu ulichukua masaa kumi na moja. Madaktari walikata Tumboni mpaka karibia na kifua pia shingoni na sehemu zingine na walifanya hivyo ili kupandisha tumbo juu na vitu vingine ili kuhakikisha wananusuri maisha yangu
No comments
Post a Comment