Wafanyabiashara wadogo madini walilia vitambulisho
Wafanyabiashara wadogo wa madini jijini Arusha, wameiomba serikali kuwatambua kwa kuwapatia vitambulisho kama ambavyo imefanya kwa wale wa biashara ndogo ndogo, maarufu kama machinga.
Wakizungumza kwa niaba ya wafanyabiasha wengine, Kalanga Mokoyo, Godson Joely na Mono Lesnga walisema kuna haja ya serikali kuwapatia vitambulisho vya wamachinga ili waweze kukusanya kodi.
Katika sekta ya madini pia, walisema kuwa watu wanamitaji midogo hivyo, wanastaili katika kundi la machinga hivyo kama itaipendeza serikali iangalie njia gani ya kuwasaidia kwa kuwa kundi la watu wenye mitaji chini ya Sh. milioni nne wako wengi.
Waliongeza kwa wafanyabiashara wenye mitaji ya kiwango hicho wako tayari kulipa Sh. 20,000 kwa miezi sita na
kwa mwaka mzima Sh 40,000, lakini kwa wale wenye mitaji kuanzia Sh. milioni saba hadi 10 wanapendekeza leseni walipe
kiasi cha Sh. 100,000 kwa mwaka kutokana na biashara kuyumba mara kwa mara.
Endapo serikali itatoa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo, walisema watakusanya fedha nyingi kutokana na wengi wao, mitaji yao iko chini ya Sh. 500,000, hivyo ni vigumu kukata leseni kutokana na mitaji waliyonayo
No comments
Post a Comment