Followers

Wajumbe wa Bodi ya JUKUMU wapigwa 'Pini' na RC Kebwe 



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amewazuia Wajumbe wa Bodi ya Hifadhi  ya Jumuiya ya Kuhifadhi na matumizi Bora ya Maliasili Ukutu (JUKUMU) wanaomaliza muda wao kutoshiriki nafasi zozote kwenye uchaguzi ujao kwa madai kuwa wameshindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yao kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Dkt. Kebwe ametoa kauli hiyo, Februari mosi, wakati akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mbwade Wilaya ya Morogoro Mkoani humu akiwa katika ziara ya kawaida ya kutembelea miradi ya maendeleo na nkusikiliza kero za wananchi.

Dkt. Kebwe amesema Viongozi hao kwa kiasi kikubwa ndio walioifikisha JUKUMU mahali ilipo kuwa na migogoro mingi isiyoisha na kwamba ili kuijenga upya jumuiya hiyo ya JUKUMU ni lazima kupata viongozi wengine wapya na waadilifu wa kuiendesha na kuisimamia.

“Viongozi wote waliokuwepo na nimepiga marufuku kama amefanya miaka kumi Katiba imekwishamuondoa, kwa hiyo hata mwenyekiti wa JUKUMU amekwishatoka kwa mujibu wa Katiba” amesema Dkt. Kebwe. “ lakini hata wale walikwisha tumikia miaka mitano wasiombe na wakiomba wasikubaliwe,” alisisitiza.

Aidha, Dkt. Kebwe hakuridhika na taarifa ya fedha ya mapato na matumizi ya Jumuiya hiyo ya zaidi ya  Shilingi 388 Mil. liyosomwa kwake kwani alisema kuna harufu ya ubadhirifu wa fedha, kwa sababu hiyo ameagiza ufanyike ukaguzi wa ndani wa mapato na matumizi ya fedha hizo watakaobainika kutumia vibaya fedha hizo watachukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Kayombe Masoud Lyoba kutuma wataalamu wake kuweka mipaka ya eneo lote la Jukumu ili iwe rahisi kwa wananchi kutambua mipaka yake na kutoingia katika hifadhi hiyo kufanya shughuli za kibinadamu.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.