Rais Vladimir Putin aahidi kushughilikia mizozo kati ya nchi yake na nchi za magharibi.
Rais wa Urusi Vladimir Putin ambaye ameshinda muhula wa nne madarakani baada ya kushinda kwa urahisi katika uchaguzi, amesema atashughulikia mizozo kati ya nchi yake na nchi za magharibi baada ya ushindi huo.
Viongozi wa kimataifa wamekuwa wakijivuta kumpongeza Putin huku waangalizi wa uchaguzi wakiripoti visa vya udanganyifu wa kura katika uchaguzi huo ambao ulijaa mivutano ya hapa na pale
Putin ameahidi atachukua hatua zinazostahili kuhakikisha mizozo iliyopo kati ya Urusi na washirika wake inatatuliwa kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia, akiongeza kwa sasa kipaumbele ni kuboresha maisha ya Warusi kupitia uwekezaji, kuboresha elimu, afya na miundo mbinu.

No comments
Post a Comment