Followers

Falsafa Tatu(3) Za Maisha Yako Na Jinsi Zinavyoweza Kukuletea Mafanikio Makubwa.

Habari mpenzi msomaji wa makala hii, na karibu katika makala ya leo. Leo tutazungumzia falsafa tatu katika maisha ambazo kila binadamu anapitia katika kipindi cha ukuaji wake mpaka pale anapokuwa mzee.
Nini maana ya falsafa?
Falsafa hutokana na maneno mawili ya kiyunani (kigiriki), yaani philolenye maana ya Upendo na Sophia linalomaanisha hekima. Kwa hiyo falsafa au philosophia ni taaluma ambayo inajishughulisha katika kutafuta ukweli wa jambo kwa njia ya kutafakari.

ULIPOTOKA, ULIPO NA UNAPOKWENDA.

 
Hizi ndizo falsafa tatu katika maisha ya binadamu
1) Falsafa ya kwanza ulikuwaje 
Ukianza kutafakari katika maisha yako ya nyuma na ulivyo sasa ni tofauti yaani ulivyokuwa mtoto na binadamu wote tulizaliwa sawa tukiwa wadogo kabisa na huku tukiwa hatuna kitu chochote katika ubongo wetu yaani maarifa wote tulikuwa sawa na mabadiliko mengi yanatokea au yanaanza kupitia hatua ya pili ya falsafa ya maisha.
Katika falsafa hii ya ulikuwaje ni falsafa ambayo kila mtu anapitia katika maisha ya binadamu hapa wote tunakuwa sawa ,lakini pale tu unapoanza kukua kila mmoja katika juhudi zake mwenyewe anaanza kujifunza mambo mbalimbali katika dunia. Falsafa hii tunaweza kusema ni kipindi cha utoto au udogo unakuwa bado hujajua nini maana ya maisha mpaka unapofikia kipindi cha kujitegemea.
2) Falsafa ya pili ukoje 
Hii ndiyo falsafa ambayo inaitwa ukoje yaani jinsi ulivyo sasa una rasilimali nguvu ,rasilimali muda nk. Hiki ni kipindi ambacho binadamu ndio anaanza kutengeneza maisha yake ukifanya uzembe katika kipindi hiki cha ujana wako huwezi kufanikiwa kipindi cha uzee wako.
Maisha ni marefu kama ukitumia muda wako vizuri, je unatumia muda wako vizuri? Katika falsafa hii ya ukoje ndio kipindi cha kuamua unataka kuwa nani katika maisha yako ,uhuru wa maisha yako unakuwa mikononi mwako uamuzi unao mwenyewe kuboresha maisha yako ili uwe na maisha bora ya sasa na ya baadae kipindi cha uzeeni. Watu wanafanya utani na muda katika maisha yao wengi wanafikiri muda upo na watakuwa na muda mwingine zaidi ya huu, Wengine wanasema bado wapo wapo muda upo kwa sasa wanakula ujana, kuja kushtuka huna tena rasilimali nguvu kama ulivyokuwa nayo kipindi cha ujana.
Watu wengi wanaopata shida uzeeni hawakutayarisha maisha yao ya uzeeni maisha yako ya uzeeni unayatengeneza sasa, ubaya ni kwamba watu wengi wanakumbuka kufanya maendeleo jua limeshazama. 
Ni hatari sana kwa mtu ambaye anafanya kazi bila kuweka akiba katika maisha yake, kutegemea chanzo kimoja cha mshahara ,bila kufanya uwekezaji, kuishi juu ya kipato chake, kuishi maisha ya starehe na anasa za dunia ni hatari pia mtu kuishi bila kujali afya yake. Afya ndio nguzo kuu ya wewe kutimiza malengo yako ,kula vyakula ambavyo vina hatarisha maisha yako kula vyakula ambavyo vinakupa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa. Kwa hiyo katika kipindi cha sasa yaani falsafa ya ukoje ni kipindi ambacho unatakiwa kuwa makini nacho hapa ndio kitovu cha mafanikio yako ya leo na kesho usipoteze muda pambana kila siku usiridhike na mafanikio uliyo nayo kwa sasa ukitaka kufanikwa kuwa kama tumbo.
Tumbo halina shukrani haliridhiki utakula sasa, mchana, usiku tena tumbo litahitaji tena kwa hiyo tumia falsafa au moto huo kutafuta kila siku bila kukata tamaa, weka malengo na mipango kwa maisha yako ya sasa na ya baadae.
3) Falsafa ya utakuwaje 
Hii ni falsafa ya mwisho katika maisha yako ambayo ni matokeo ya falsafa ya pili. Kama uliweza kutumia muda vema katika ujana wako hapa ndio kipindi cha kuvuna utakuwa unakula matunda yako mwenyewe ambayo ulijiwekezea kipindi una nguvu za kutosha ,kila mtu anaishi katika maisha aliyojitengenezea mwenyewe na kila mtu anaishi katika dunia aliyojitengenezea . Hiki ni kipindi ambacho umeshazeeka huna tena nguvu za kuzalisha nguvu ya kufanya kazi kama awali kama ulikula ujana vibaya hapa pia utakula uzee vibaya maisha yatakuwa magumu sana uzeeni kama ulishindwa kuyaandaa kipindi cha ujana. Maisha ni muda. Mafanikio yanatabirika kama vile jua linavyochomoza mashariki na kuzama magharibi.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.comau unaweza kutembelea tovuti yake

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.