Followers

Gideon Moi atangaza rasmi azma yake ya kuwania urais 2022


Seneta wa Baringo, Gideon Moi ametangaza rasmi azima yake ya kuwania urais mwaka wa 2022


Gideon alisema kuwa yuko tayari kufuata nyayo za babake mzee Daniel Moi ambaye alikuwa rais wa pili wa nchi hii


Vile vile wanachama wa KANU walimhimiza Gideon kuwania kiti hicho na kuhakikishia kwamba watamuunga mkono ifikapo mwaka wa 2022


Seneta wa kaunti ya Baringo Gideon Moi alitangaza rasmi Jumapili Aprili 8 kwamba amejiandaa vilivyo kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Seneta wa Baringo, Gideon Moi ametangaza rasmi azima yake ya kuwania urais mwaka wa 2022.Picha: Abdulla Dido


Gideon alisema kuwa anataka kufuata nyayo za babake ambaye alikuwa rais wa pili wa nchi hii kwa miaka 24.


TUKO.co.ke iliweza kubaini kwamba Gideon alitangaza habari hizo akiwa katika makaribisho ya mbunge wa Tiaty, William Kamkatet.


Wananchama wa KANU waliokuwa kwenye hafla hiyo walimrai Gideon kuwania kiti hicho bila tashwishi na kwamba watamuungano mkonao katika uchaguzi huo.


Uamuzi wa Moi unatokea baada ya wanasiasa kadhaa kutofautiania kuhusu atakaye riuhusiwa kuwania kiti hicho ifikapo 2022.

Seneta wa Baringo, Gideon Moi ametangaza rasmi azima yake ya kuwania urais mwaka wa 2022.Picha: Uhuru Kenyatta/Facebook


Hata hivyo, kumekuwa na tetesi kwamba huenda Rais huru Kenyatta akamuidhinisha Moi kuwa mridhi wake ikizingatiwa kuwa familia yake na rais mstaafu, Daniel Moi ina uhusiano wa karibu sana.


Gideon sasa atatarajiwa kumenyana na naibu rais William Ruto, aliyekuwa gavana wa Kiambu, William Kabogo, gavana wa Machakos, Alfred Mutua na kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka.


Habari za kuaminika ziliarifu kuwa, Gideon yuko na matumaini kwamba Uhuru atamuachia nafasi hiyo na yuko tayari kuwahudumia Wakenya.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.