Followers

Haiwezekani Majuto asumbuke hivi;Serikali




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema inaudhi kuona msanii wa filamu, Amri Athuman maarufu King Majuto anaomba msaada wa Sh 500,000 kwa ajili ya matibabu wakati kuna makampuni yalifaidika naye kwa kuingia mikataba aliyodai ya dhuluma.



Kutokana na hali hiyo, amesema serikali imechoka kusikia vilio vya wasanii wa filamu kudhulumiwa haki zao na sasa imeunda kamati maalumu ya wanasheria kukagua mikataba yote ya mashirika na makampuni waliyoingia wasanii akiwamo  King Majuto na marehemu Seteven Kanumba ‘Kanumba’.



Pia imeagiza wasanii wote ambao wanaona wameingia mikataba ya kipumbavu na makampuni au mashirika hayo wawasilishe taarifa zao kwa serikali.



Dk. Mwakyembe amesema hayo jana  Aprili 27, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge katika kuhitimisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo.



“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana Watanzania wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa- empower (kuwezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wasitumie middle men.



“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu,” alisema Dk. Mwakyembe.



Alisema licha ya kwamba nusu ya mabango ya biashara na matangazo ya biashara ni ya  Mzee Majuto inashangaza kuona anaomba fedha ya matibabu.

DOWNLOAD APPLICATION YA SUPERNIDA KATIKA SIMU YAKO ILI UWE UNAPATA HABARI KWA ULAHISI ZAIDI 
DOWNLOAD HAPA

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.