Followers

Irene Uwoya, Dogo Janja Baada ya Kifo cha Masogange Waikimbia Nyumba



STAA  wa filamu Bongo, Irene Uwoya na baby wake Abdul Chende ‘Dogo Janja’ wamefunguka dhamira yao ya kuihama nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu Agness Gerald ‘Masogange’ iliyopo Makongo Juu jijini Dar wakidai kuwa, hawatakuwa na amani.


Agnes Masogange ambaye alikuwa video queen katika nyimbo kadha wakadha ikiwemo ya Belle9 inayo kwenda kwa jina lake hilohilo la masogange.


Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa niaba ya mkewe, Dogo Janja alisema kuwa hawawezi kuendelea kuishi hapo tena kwa sababu kwao itakuwa ni majonzi kila siku na hiyo ni kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa Masogange.


“Kwa kweli mimi na mke wangu hatuwezi tena kuendelea kuishi Makongo Juu kwenye ile nyumba maana kwetu itakuwa ni simanzi tuu, Masogange alikuwa ni mtu wetu wa karibu sana na tulikuwa tukifanya vitu vingi pamoja, pia mke wangu atakuwa na huzuni sana akiendelea kuishi pale,” alisema Dogo Janja.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.