Followers

Hizi Ndizo Dalili za Mtu mwenye Mawe katika Figo



Figo ni kiungo muhimu katikamwili wa binadamu, hufanya kazi ya kuchuja damu huku ikiondoa sumu zote za mwili ,figo hufanya kazi ya kurekebisha kiasi cha maji mwilini (electrolyte level).

Kabla damu haijapita katika figo, huwa imebeba maji na taka taka nyingi sana (urea) ,lakini inapopita katika figo huchujwa na vitu muhimu hurudishwa katika mzunguko wa damu lakini,masalia mengine ambayo hayafai tena katika mwili ikiwani pamoja na kiwango cha maji kilichozidi hupitishwa kwenye mirija miwili (ureters)kuelekea kwenye kibofu ( urinary bladder) nakisha  kutolewa nje ya mwili kupitia njia ya mkojo (urethra).

Mkusanyiko wa kemikali hizi (chemical crystals), wakati mwingine hugandamana na kutengeneza chembechembe ya vitu kama mchanga,kadri siku zinavyozidi kuendelea ndivyo vinavyozidi kukua hadiwengine hufikia hatua ya kuziba njia ya mkojo katika figo yenyewe (neprone) au kwenye mirija yakupeleka mkojo kutoka kwenye figo kwenda kwenye kibofu (ureteter), hapo ndipo mtu anaanza kupata shida ya kukojoa na kusikia maumivu makali.

Hizi dalili kuu za uwepo wa mawe katika figo:

Mtu mwenye mawe kwenye figo huonyesha dalili zifuatazo;

1. Maumivu ya mgongo na kiuno
2. Mkojo kutoka ukiwa na rangi ya damu
3.Kutokwa na jasho wakati wa usiku
4. Kupatwa na homa kali kwa wakati flani ikiambatana na kutetemeka mwili
5. Kuhisikichefuchefu na kutapika
6. Mkojo kuwa na harufu kali
7. Maumivu makali sehemu za mbavu
8. Miguu kujaa maji/kuvimba.
9. Maumivu ya tumbo chini ya kitovu upande wa kushoto au kulia kutegemea ni figo ya upande gani iliyoathirika.
10. Maumivu makali unapogusa upande wa figo iliyoathirika.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.