Followers

JPM ÀWEKA WAZI LENGO LA SERIKALI ANAYO IONGOZA




Rais Dkt. John Magufuli amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Iringa kwa kuweza kupata barabara ya uhakika na kuwataka kuongeza juhudi katika uzalishaji mali hasa katika kilimo na biashara ili waweze kunufaika nayo nasio vinginevyo.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo Aprili 29, 2018 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa barabara ya lami ya kutoka mkoani Iringa kuelekea Migoli hadi Fufu yenye urefu wa kilomita 189 na ambayo inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma.

Dkt. Magufuli amesema pamoja na kujenga barabara hiyo, serikali inauboresha uwanja wa ndege wa Nduli ili uweze kupokea ndege kubwa zitakazoweza kupokea watalii wengi na wafanyabiashara katika mkoa wa Iringa na maeneo mengine ya kusini mwa Tanzania ili rasilimali zilizopo katika maeneo hayo ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ziwanufaishe wananchi kama wanavyonufaika wananchi wa Kaskazini mwa Tanzania. 

“Ruaha ni hifadhi kubwa, nataka hifadhi hii iwe kitovu cha utalii, nataka nyinyi ndugu zangu wa Iringa mnufaike na utalii katika hifadhi hii kama wanavyonufaika kule kaskazini kupitia Serengeti, watalii wakija hapa wenye hoteli watapata wateja, wenye maziwa watauza, wenye matunda watauza, wenye mahindi watauza, mtapata hela”, amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewataka wananchi wa Iringa kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa sana, na kueleza kuwa fedha hizo hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa muda mrefu, na kwamba ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kuchochea uchumi wa Taifa letu

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.