Followers

Mama Mzee Asimulia Kisa Cha Kweli "Kizuri"

Asema: Nilikua Na Watoto Watatu Na Wote Wameoa.. Basi Siku Moja Nikamzuru Yule Mkubwa Na Nikataka Nilale Kwake, ilipofika Asubuhi Nikamwambia Mke Wake Anipe Maji Ya kutawadhia... Nikatawadha Vizuri Nikasali Kisha Yale Maji Yaliobakia Nikayamwaga Katika Kitanda Nilicholala... Mke Wa mtoto Wangu Aliponiletea Chai ya Asubuhi Nikamwambia Ewe Mwanangu Hii Ndio Hali Ya Watu Wazima Nimekojoa Kitandani, Mke Akakasirika Na kunifyokea Na Kunitolea Maneno Mabaya Kisha Akaniambia Nioshe mashuka Niyakaushe Na Nisirudie Tena Kufanya Hivyo... Bibi Asema: Nikajifanya Naficha Hasira Zangu Nikaosha Tandiko Na kuikausha... Kisha Nikaenda Kulala Kwa Mwanangu Wa pili Nikafanya vile vile, Mke Wake Akaja juu Na kupiga Kelele Na kumueleza Mume wake Ambaye ni mwanangu Na hakumkemea... Nikatoka kwao Nikaenda kwa Mwanangu Mdogo... Huko Nako Nikafanya vile vile Mke wake Aliponiletea Chai ya Asubuhi Nikamweleza kwamba Nimekojoa Kitandani... Akasema: Usijali Mama... Hii Ndio Hali Ya Watu wazima... Mara Ngapi Sisi Tulikojolea Nguo Zenu Tukiwa watoto... Kisha Akachukua Zile Nguo Na Kuziosha Na Kuzisafisha...Nikamwambia.Ewe Mwanangu Mimi Nina Rafiki Amenipa Pesa Nimnunulie Mapambo Ya wanawake Na sijui Kimo Chake Lakini Anamwili kama Wako... Nipe kipimo Cha mkono wako.. Bibi Akaenda Sokoni Na kununua Dhahabu Kwa Mali Yake Yote... Na Bibi Alikua Na mali Nyingi... Kisha Akawaita watoto wake watatu Pamoja Na wake Zao Nyumbani Kwake Kisha Akatoa Zile dhahabu Na yale Mapambo.. Akawasimulia Kua Yeye Ndie Aliemwaga Maji Kitandani Na haikuwa Mikojo... Kisha zile Dhahabu Akaziweka Mkononi Mwa Mke Wa Mtoto Wake Mdogo Na Akasema Huyu Ndie Binti Yangu Ambao Nitaenda Kwake Nikiwa Mkongwe... Na Ambaye nitamaliza Kwake Umri wangu Uliobakia... Wale wake wawili wakapigwa na Butwaa Wakajuta Majuto makubwa..

Ukifurahishwa Na hiki kisa watumie uwapendao ili wajifunze

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.