Followers

Mambo ya kuzingatia kwa wanaume wenye umri chini ya miaka 45

Habari wakuu,
Kuna kitu nimeona tuhabarishane kidogo hasa sisi vijana na wanaume watu wazima chini ya umri tajwa hapo juu. Ni vitu vya msingi sana katika maisha yetu ya kila siku katika nyanja zote.

1. MTANGULIZE MUNGU KWA KILA JAMBO
Kama unaamini Mungu basi muweke mbele kwa kila jambo lako. Ni siri ya mafanikio ya watu wengi sana. Usichoke.

2. LINDA AFYA YAKO
Afya njema ni mtaji, hakikisha unailinda kwa nguvu zote. Epuka sana vitu vitakavyosababisha kuharibika afya yako in both short and long run. Sihitaji kusema ni vitu gani vinaharibu afya.

3. JIFUNZE SELF DEFENSE
Hapa ni muhimu kuwa na mbinu kadhaa za kuweza kujiokoa unapopatwa na jambo gafla kama kuvamiwa na vibaka. Kuwa na idea ya stance na hata kurusha ngumi na teke ( karate ) au hata boxing. Juwa kukwepa kitu kama kisu kinachoelekezwa kwako. Mwanaume usikae kindezi ndezi tu. Mi ninaamini yule bwana aliyevamiwa na scorpion Buguruni kama angekuwa anajua style mbili tatu basi angeweza kujitetea.

4. JIFUNZE KUENDESHA VYOMBO VYA MOTO
Kuwa mjanja. Hata kama huna gari au pikipiki na vema kujua namna ya kuviendesha vyombo hivi vya moto. Ni muhimu sana. Kuna siku utahitajika kufanya hivyo ukaishia kupata aibu au kushindwa kutoa msaada. Hakikisha una leseni husika pia.

5. JIFUNZE NA MASTER KUFANYA KAZI NDOGO NDOGO NYUMBANI
Kuna bulb imeungua, mwanaume huwezi hata kupachika nyingine. Ni aibu. Mke, demu wako anaosha vyombo mara sink limeachia anakuita uje ucheki kijana huwezi fanya chochote. PC ya mtoto imezingua mtu wa kwanza kukuambia ni wewe. Fanya kitu. Kuwa na idea, likikushinda kabisa ndio uite fundi. Ndani kwako hakikisha una set ya screw drivers pliers, n.k kukabiliana na vitu kama hivyo.

6. TAFUTA PASSPORT
Unaweza kosa deal la maana kisa huna passport. Hii ni sambamba na kukosa deal kisa huna leseni ya kuendesha gari. Mjini mipango. Jipange.

7. KUWA FAMILIAR NA MAMBO YA KITABIBU NA SHERIA
Hapa simaanishi ukasome medicine wala school of Law. Wewe kuwa na idea ya aina ya magonjwa, vifaa tiba, madawa n.k. Fahamu sheria muhimu zinazotugovern katika maisha yetu ya kila siku. Leo ukimuwa UTI, daktari akakupa dawa na kesho ukaumwa tena ukapewa zingine. Jitahidi kujua ni kwanini na uwe na idea. Mimi binafsi nina rafiki yangu wakati tunaanza kufahamiana alidhani nimewahi kusoma clinical medicine kwa jinsi nilivyokuwa namueleza nikijisikia vibaya. Yeye ni daktari.

8. TAFUTA SANA PESA NA ZITUMUE VIZURI
Ndio. Tafuta pesa na uzitumie vizuri. Kuna uhusiano mkubwa wa pesa na shetani. Lakini kama Mungu atakuwa yuko nawe utakuwa upande salama. Ndio maana nimeweka hili jambo la mwisho. Lingeweza kuwa la pili hapo juu.

Asanteni.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.