Followers

Mawandaz.Tuwe makini na mitandao ya kijamii

Picha/Video Wakati wa Faragha.!

Wadau wapenda mahusiano,mapenzi na urafiki habarin za usku?

Nimeingia mda huu Jf kiukwel ni kutokana na story ya Star mchanga kabsa "Nandy" kuibua mjadala mkubwa katka "social network" nyingi sana nchini na nchi za nje za majirani zetu, kiukwel kitendo alichokifanya cha kuachia post ya vdeo fupi "clip" akiwa yy bnafs faragha na msanii mwenzie Billnas imeumiza watu wengi sana hasa tukiamin kwa Tanzania bado ni vitu vgen kijamii ingawa kimmoja mmoja ni kawaida sana.
Nasema kuachia yy nkiwa na maana kuwa yy kama yy kwny video ndio anaonekana kurekod ile vdeo kwa bashasha kbsa lakn kwann ije kurushwa na mtu mwngne mitandaoni???
Kwny hili nafikir naweza kuliangalia ktk namna mbili tatu hv

1. Namna ya kwanza kwanza ni kwa Nandy kutaka kuwafanyia surprise waTz kuwa Billnass ni mpenz wake na pengne hii inakuja kutoka na amesikia labda Billnenga kama anavyojiita kuwa anatoka na msichana mwngne ambaye kwa vyvyote ni msanii mwenzake hta yawezekana ni shosti yake kwhyo imetumika trick ichukuliwe video fupi halaf Nandy atulie aje aitupie Billnas Insta nakuaminisha watu kuwa yy hakufanya kwakuwa haikutokea kwake na pengne aliiogopa zaid familia yake lakn akashndwa kufikir mbinu nzr ya kumthibitishia mbaya wake kwa yy yupo na Billnass kama wapenz.

2.Namna nyingne ni pale ambapo nakumbuka ni juzjuz tu wik za karbun Nandy alihojiw juu ya mahusiano yke na Billnas na akakataa katakata juu ya mahusiano yao, sasa tuamin kuwa ni kwel Hana mahusiano nae kwa sasa labda waliachana kwahyo tuchukulie Billnas akaamua kuonesha video ile ili waTz wajue kuwa Nandy ni muongo na hakusema ukweli juu mahusiano yao. Hivyo kwa video ile kuipost itamlazmu Nandy awe Punda kwa Billnas kwasabab pengne Nandy anajua kuna vtuko vingi alishafanya na Billnas kipnd wapo ktk mahusiano na anaamin vkirushwa kwa awamu itakuwa balaa kuanzia kwa familia yake,heshma yke na kazi yake kwa maana muziki wake. Kwahyo hii ndio inamfanya awe yupo "stress" zaid ya tukio lenyewe,ambapo itamlazmu kufuata matakwa ya Billnas pengne waendelea na mahusiano kama hayapo kwa sasa.

3.Namna ya tatu ni "Masuala ya kibiashara" pengne kuna watu wameamua kufanyia kazi na kuratb kila ktu juu hili jambo na hii ni baada ya kuona kuwa Nandy yupo juu pale kimuziki na asiweza kushuka Leo au kesho na muziki ni biashara ngumu kwa sasa na ghali Tz, hivyo wakaamua kuratibu hili na kulifanya liwe jambo kubwa la kumnyongonyeza Nandy katka kazi zake na kumtoa kwenye reli na hvyo kutoa nafas kwa wadada wengne kupata airtime kwny media za bongo hapa Tz, so kama ni hvyo bas lazma Billnas atahuska juu ya hili kama sehm ya ushiriki wa kushusha heshima ya mtu tena kwa mambo ya faragha.

Nini kifanyike baada ya khasia hii:
a)Kwanza ni kuhakikisha Jamii inaachana na tabia hii ya kujirekod wakati wa FARAGHA au kujipiga picha haina mantik halisi yan wapenz mkishakubaliana mpo faragha bas yapo mambo mengi ya kufanya lakn sio kitandan upande na camera au simu yan hta hao porn stars wakitaka kufanya movie zao wanakuwa wanajua ni uhalisia ndio maana inakuwa vle lakn siamin kupga pcha na video ni sehm ya kuamsha hisia na ukiona una mpnz wa kupga pcha ndio aamshe ujue hapo una kanyaboya, sikatai kwel unawez ukapga pcha na mpnz faragha lakn bas iwe kpnd cha awali mmeingia tu bado hta kuanza chchote bas hpo ni sawa lakn sasa ww mtu tayar kitandan mchupi huo kwa kamera haifai.

b) Ikiwa Nandy kwel anayojitetea ana hakika ni kweli kabsa basi nafikiri mm sio mwanasheria lakn naamin akifuata protocal za kimahakama atapata nafas nzuri ya kupata haki yake ya "kuheshimiwa" ambayo imepotezwa ndan ya sekunde chache sana na watu au mtu akishiriki kupost video ile kwa Mara ya kwnza mtandaoni hapa ndio ile sheria yetu chungu itafanya kazi kwa uhakika na wataadhibiwa wahuska wa kosa hilo.

c) Kuna kitu huwa tunakisahau sana jmn ktk industry ya mziki nacho "manager wa msanii" hyu ni mtu muhimu sana ndiye dira ya msanii huska yan watu kama hawa inapotokea msanii ameharbu kama hivi mtu wa kwnza kumshambulia ni meneja wa msanii lakn sasa kwa bongo utagundua wasanii wengi wapo tu wakiamin game wanaweza kuismamia wrnyew hapana tuwaelimisheni kuwa msanii lazm uwe "under management" ili kuleta mafanikio karb na ww. Niliwahi kuuliza baadhi ya wasanii kwann huna meneja akanijib kuwa " mameneja wanataka pesa ndefu wakati mm nalipwa laki NNE au Tano kwhyo stawez mm ntalisongesha hvohvo" nkajua tatzo lipo kwa watu wanaisimamia mziki kuwa hawakuwaanda mameneja weng kwa hyo wanazidiwa na wasanii.

Naomba tujikute tunakataa kufnya mambo bila kufikir vyema athari zake hii inatupa funzo kuwa kabla yakufnya jambo lolote hakikisha umetafakari vya kutosha kujua "uchanya na uhasi" wake ili uone wap utasimamia baada ya matokeo.
Tusiwe wepesi wa kulaumu na kujuta kwa mambo tuliyokwisha yafanya tena yakionesha MAANDALIZI KABISA kama tulikaa tukafikir na tukaamua kutenda.
Niwape pole wote hasa Familia ya Nandy lakn pia mashabiki wake na mm nkiwepo kiukweli wapo watu waliosema sitaki kuangalia wala kuskiliza tena nyimbo zake hyu binti lakn tatzo ni kwamba 85% ya mashabiki walimchukulia Nandy binti Mdgo mchanga Sana aliyefanikiwa haraka kutokana na kipaji chake lakn wakasahau yy ni bnadamu kama walivyo wengne hvyo sifa ya ukamilifu wa bnadamu ni UKOSEFU hvyo tukabali jaman Nandy amekosea kama bint yyte anavyowez kukosea ktk Jamii tumsapoti tukimuacha hpa kwa sasa kwa maana ya kumzira basi tutakuw tumzima kama mshumaa uliweka ufukweni.
Usku mwema.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.