MAMA mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo, Bi. Rehema Paulo Momburi amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Aprili 13, 2018 katika Hospitali ya The Madras Medical Mission – Chennai nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Akitoa taarifa hiyo, RAS wa Arusha amesema;
“Ninasikitika kuwataarifu kifo cha Bi Rehema Paulo Momburi mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa Arusha, Bw. Mrisho Mashaka Gambo, kifo kimetokea usiku wa kuamkia leo 13/4/2018, huko Hospitali ya Madras Medical Mission Chenai India, mipango ya msiba mtajulishwa baadaye.”
No comments
Post a Comment