Mimi na Mume Wangu Hatugombani kwa Sababu Natambua Majukumu Yangu-Martha Mwaipaja
Msanii wa nyimbo za injili Tanzania martha mwaipaja amefunguka na kusema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakishindwa kutulia katika ndoa zao kwa sababu wanakuwa hawatambui majukumu yao katika ndoa zao.
Martha anasema kuwa kila mtu anamajukumu yake katika maisha ya ndoa na jambo zuri ni pale ambapo watu hao wanakuwa wanaelewa majukumu yao na kuweza kuyatekeleza .akitolea mfano wa ndoa yake na mume wake , Martha anasema kuwa
“mimi na mume wangu hatugombani kwa sababu natambua majukumu yangu kama mke, unajua watu hawajui kuwa kiasili mungu amemuweka mwanaume kuwa mtawala, amtawale mwanamke sasa ugomvi mwingi unatokea pale mwanamke anapotaka kuwa jeuri , kubishana na mwanaume”
Martha anasema kuwa jambo kubwa mwanamke anachotakiwa kujua ni kwamba mwanamke yuko chini ya mwanaume hivyo ugomvi mwingi katika ndoa utokea kwa sababu mwanamke anataka kuwa jeuri na kumbishia mwanaume.
No comments
Post a Comment