Followers

Nandy aomba radhi baada ya video yake kuvuja

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nandy ambaye leo Aprili 12, 2018 imesambaa kwenye mitandao ya kijamii video yake ya utupu inayomuonyesha akiwa faragha na msanii mwenzake Bill Nas. ameomba radhi kwa wazazi wake, serikali, jamii pamoja na kanisa lake juu ya video hiyo.

Nandy amesema video hiyo ni ya mwaka 2016, na haelewi kwa nini mtu aliyeivujisha kaamua kufanya hivyo, lakini ni kitendo kilichomuumiza sana hivyo anaomba msamaha kwa jamii, mashabiki, kanisa na kila mtu ambaye imemgusa kwa namna moja au nyingine wamsamehe, kwani tayari anajutia jambo hilo.

“Nimesikitika sana, hiyo video ni ya ukweli ni ya mwaka 2016, nilikuwa na mahusiano na Bill Nas na tulikubaliana iwe siri, sasa sielewi kwa sababu gani kaamua kuvujisha, nimesikitishwa sana, ni video ambayo ilishutiwa kwa snapchat, sasa sielewi wakati ameipata hiyo video alikuwa nayo au alichukua mwenyewe, sijui niseme nini, naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, serikali yangu, mashabiki, naomba radhi sana, adhabu ya maumivu ambayo nayapata imetokana na kumuamini mtu, ilikuwa ni private”, amesema Nandy.

Nandy, ni msanii wa kizazi kipya anayefanya vizuri kwa sasa huku kwa upande wa Bill Nas naye akitikisa kutokana na nyimbo zake mbalimbali alizotoa.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.