Followers

Mlinzi wa aliyekuwa kamishna wa IEBC, Paul Kurgat apigwa risasi na kuuawa

Afisa wa polisi kutoka kikosi cha Recce na ambaye amekuwa akimpa ulinzi kamishna wa zamani wa IEBC ameangamia baada ya kupigwa risasi na majambazi

Alikuwa amejaribu kuwaua majambazi waliokuwa wamevamia basi alimokuwa, ila wakamzidi nguvu na kumuua

Afisa mmoja wa GSU kitengo cha Recce na ambaye amekuwa akimpa afisa wa zamani wa IEBC, Paul Kurgat ulinzi ameuawa na majambazi akijaribu kuwalinda abiria.

Kulingana na maafisa wa polisi, majambazi hao walimpiga risasi na wakitumia bunduki lake kabla ya kutoweka nalo.

Mlinzi wa aliyekuwa kamishna wa IEBC, Paul Kurgat apigwa risasi na kuuawa PICHA: Hisani

Majambazi hao pia walimpiga risasi abiria mwingine kwa gari kwa tumbo, wakimwacha katika hali mahututi katika tukio hilo la Jumamosi, Aprili 28, katika barabara kuu la Thika.

Paul Kurgat ambaye afisa aliyekuwa aimpa ulinzi aliuawa PICHA: Hisani

Afisa huyo alikuwa akisafiri kutoka Ruiru hadi makao makuu ya GSU wakati majambazi hao waliokuwa wamejifanya kuwa abiria walianza kuwapora abiria wengine.

Afisa huyo alitoa bunduki lake na kupiga risasi mara moja tu kabla ya majambazi hao kumshinda nguvu, na kumuua wakitumia bunduki lake.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.