Followers

Mzee Majuto kupelekwa India kupata matibabu


Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Steve Nyerere kwa Pamoja wamekwenda hospitali aliyolazwa muigizaji mkongwe mzee Majuto kwa lengo la kumuona na kumpa faraja katika kipindi hiki ambapo amelazwa katika hospitali hiyo.

Pamoja na kwenda hapo wamemkuta Mzee Majuto yupo kwenye hali nzuri huku akijitokeza mdau ambaye ni Kampuni ya ASAS aliyejitolea Ticket mbili kwaajili ya Mzee Majuto kwenda kutibiwa India.

Baada ya hapo Msanii Steve Nyerere alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa….>>>“Ni kweli tumepata ticket mbili za Mzee wetu kwenda kutibiwa India na siku ya kesho tutakamilisha huo utaratibu wote na sisi tunajaliana kwenye shida tuache haya makundi ya ajabu ajabu kama tunataka kutengeneza Industry lazima tukubaliane wote tuache porojo hazijengi Industry ila zinakandamiza” – Steve Nyerere

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.