Followers

Nilimtesa aliyekuwa ananipenda sasa najuta baada ya kuvunja uhusiano na mimi

Nimeamini chozi la mwanamke haliendi bure niliwahi ku take advantage kwa mwanamke aliekuwa ananipenda kwa dhati sio siri nilikuwa nampa mawazo sana na hana la kufanya kwasabab kafa kaoza nilikuwa na mcheat sana na mademu tofauti

Kipindi hiko nilikuwa siwezi kujizuia na vishawishi kutokana na shughuli nilizokuwa nafanya mwanamke alinipenda mpaka kwetu pia walikua wanamjua kifupi ni mwanamke ambae alikuwa permenent kwangu kuna zile unazungukaaa lakini unajua kuna mtu huwezi kuachana nae.

Nilikuwa naamini hawezi kuniacha na mima siwezi kumuacha hata iweje ndo mtu niliepanga kuanzisha nae familia kashanifumania lodge na mwanamke asubuhi asubuhi nimelewa chwiii hata sijielewi lakini akanisamehe maisha yakaendelea.

Lakini nilikuwa na kimchepuko kangu ni kazuri haswa yaani nikisema mzuri jua ni mzuri halafu ni fundi balaa kitandani alikuwa ananipa kila ninachotaka ambapo upande wapili sipewi yani ilifika hatua naweza nisi sex na mpenzi wangu nikaenda kwa mchepuko nazuga nasafiri na chaji nasahau makusudi ili simu ikizima niwe na cha kujitetea.

Tunafanya ushetani nikirudi kwangu nimechokaa hoi hata mpenzi wangu akaaje simtamani basi yule mpenzi wangu ilifikia anampgia simu mama yangu anamuelezea uchafu wangu basi nikawa namchukia kwanini amshirikishe mama kumbe mimi ndo ninamakosa na mpaka rafiki zangu walihisi nimerogwa na yule mchepuko

Kwasababu nayeye mchepuko alikuwa ananiendesha balaa sisikii lakini akinuna tu nakuwa sijisikii poa nta go extra mile awe sawa hakuna asichopata kwangu.

Lakini mimi ndo nilikuwa napata tabu sana kwasababu alijua nampenda akaanza kuniendesha nikawa kama chizi akawa ananipimia yaani mpaka ajisikie yeye basi mi nachukia lakini ntafanyaje?

Mpaka siku moja nikapata matatizo usiku nivyotoka na huyo mchepuko ukatokea ugomvi nikakamatwa na polisi nikalala siku mbili kituoni

Huwezi aminii yule mpenzi wangu ndo alopambana mpaka nikatoka na yule mchepuko alikimbia mji kwa sababu alikuwa anatafutwa na polisi alimpiga mtu na chupa ya bia kichwan huyo mtu alichanika sana.

Baada ya tukio hilo pia huyo mpenzi wangu akanisamehe na nikampromiss sitarudia tena na kweli from there niliacha kabisa ishu za wanawake kabisa nikawa nafocus kwake.

Cha ajabu rafiki zake wakaanza kumjaza upepo like mimi sio mtu sahihi kwake ni vilio kila siku so wakamshauri aniache kwa sababu yeye ni mzuri hivyo atapata mwanaume sahihi Kweli yule bibie akaamua kusitisha mahusiano nikaona ananitania kumbe alikua anamaanisha..

Nikaamini kuwa mwanamke akichoka anakuwa amechoka kweli basi nikachezea block kila sehemu na hakutaka tena kuonana na mimi kwasababu aliamini tungeendelea kuwa karibu angenisamehe.

Kiukweli najuta na nimeona nimepoteza sana wakati na mpaka leo hii nipo single sasa ni mwezi wa sita tangu ameniacha nasiachi kumkumbuka na kumuota mara kwa mara
niliamua kumtafuta na kumuomba msamaha hata tuwe marafiki lakinialikataa hataki hata kuniona na rafik zake wote wamenichunia.

Jamani wanaume wenzangu kama kuna mwanamke wako anakupenda na mmetoka mbali nawasihi wapeni mapenzi yanayostahili

Msi take advantage chozi la mwanamke haliendi bure ipo siku utalipa na utajutia maisha yako yote nimempoteza ninae mpenda kwa ujinga wangu mwenyewe na wala sina wa kumlaumu.

No comments

Theme images by sandoclr. Powered by Blogger.